Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya akizungumza kwenye ufunguzi wa Kambi ya madaktari inayoendelea katika viwanja vya Hospital ya rufaa ya Mkoa Sekoutoure
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bahati Msaki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ufunguzi wa kambi ya madaktari bingwa
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye Kambi ya madaktari bingwa iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekoutoure wakichukuliwa vipimo mbalimbali kwaajili ya uchunguzi wa afya zao
***************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi Mkoa wa Mwanza na Mikoa jirani wametakiwa kujitokeza kupata huduma za kimatibabu za magonjwa mbalimbali katika kambi ya madaktari bingwa iliyopo katika hospital ya rufaa Sekoutoure.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya, katika ufunguzi wa kambi ya madaktari bingwa kutoka hospital ya Kanda ya Bugando na hospital ya rufaa sekoutoure.
Balandya ameeleza kuwa Hospital ya Sekoutoure imeendaa kambi hiyo ya madaktari bingwa Kwa lengo la kutoa huduma na kuwasaidia wananchi kutambua afya zao pamoja na kupata matibabu Kwa gharama nafuu.
“Kambi hii itakuwa na madaktari bingwa Kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali Kwa wananchi za uchunguzi ili kuweza kufahamu afya zao” Alisema Balandya.
Amefafanua kuwa madaktari Bingwa waliopo katika kambi hiyo Kwa ajili ya kutoa huduma ni pamoja na Daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na uzazi, Watoto, Macho, Meno, Mionzi, magonjwa ya damu, mfumo wa chakula, magonjwa ya akili, huduma ya kusafisha damu, huduma za mahabara na dawa.
Aidha ameongeza kuwa kutakuwa na vipimo mbalimbali vitakavyotolewa hospitalini hapo Kama vile, Vipimo vya kisukari, vidonda vya tumbo, x-ray, moyo, Figo pamoja na magonjwa ya damu Kama vile, selimundu, Kansa ya damu, mchafuko wa damu mwilini.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya rufaa ya Mkoa Sekoutoure Bahati Msaki, ameeleza kuwa wamewaleta madaktari bingwa ili wananchi waweze kuchunguza afya zao na kubaini Kama Wanamagonjwa yoyote ili waweze kupata Kinga kabla ya ugonjwa haujaleta madhara makubwa mwilini.
” Nawasisitiza watu waje ili wapime na wafahamu afya zao kwani afya ndio mtaji wako ukiwa na afya njema utaweza kufanya kazi zako vizuri” Alisema Bahati.
Mariamu Mussa na Ibrahim limo ni baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma katika kambi ya madaktari bigwa wameishukru serikali Kwa kuweka kambi hiyo kwani wamepata huduma Kwa haraka na gharama nafuu.
” Tunaiomba serikali kuweka utaratibu wa kuleta huduma hizi mara mbili Kwa mwaka Kwa sababu inasadia kupata huduma hii Kwa wakati” Walisema.