Akiwa nchini Ufaransa kwenye Mkutano wa Bodi Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE) ambayo yeye ni Mwenyekiti, Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazunguzo mafupi na Mheshimiwa Amadou Ba, Waziri Mkuu wa Senegal. Katika mazungumzo hayo, masuala ya elimu yaligusiwa, kati ya masuala mengine.
Akiwa nchini Ufaransa pembeni ya Mkutano wa Bodi Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE) ambayo yeye ni Mwenyekiti, Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazunguzo mafupi na Bi. Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Katika mazungumzo ya viongozi hao, imekubaliwa kuwa UNESCO na GPE zitaendalea kushirikiana katika kupeleka ajenda ya elimu ya mbele.