Ibrahim Ngwada akimkabidhi ngao ya kutambua mchango wa kukuza elimu ya nyimbo za utambaduni mwalimu Frola Paul Nyamahanga kwa kazi nzuri ya kufundisha wanafunzi. Na Fredy Mgunda, Iringa.
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kuwa watumishi wa Halmashauri hiyo watakao fanya kazi kwa weredi na ubunifu mkubwa wanatakuwa wanapewa Motisha ya fedha kila wakati.
Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri cha robo ya mwaka 2022/23 hicho, Ngwada alisema kuwa sasa imefika wakati kwa kila mtumishi atakaye kuwa anafanya vizuri lazima apewe fedha na cheti au ngao kwa ajili ya kumuongezea morali ya kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.
Ngwada alimtaja mwalimu Frola Paul Nyamahanga amekuwa mwalimu anayejituma kufundisha wanafunzi masomo ya kawaida na michezo ya kitamaduni ambayo kwa kiasi kikubwa michezo hiyo ambayo amekuwa haipewi kipaumbele.
Alisema kuwa mchezo wa ngoma umekuwa mchezo pendwa wakati wa matamasha mbalimbali ya serikali na ambayo sio ya kiserikali lakini mchezo umekuwa ukiburudisha watu wengi.
Ngwada alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inampongeza mwalimu Frola Nyamahanga kwa kuendelea kufundisha wanafunzi michezo ya kitamaduni ambayo imekuwa haipewi kipaumbele kwa jamii.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilimkabidhi mwalimu Frola Nyamahanga Ngao pamoja fedha kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kumuongezea morali ya kufanya kazi ya kuwafundisha wanafunzi michezo ya kitamaduni.
Katika hatua nyingine Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa wanampatia kiasi shilingi million moja afisa ustawi wa jamii Tinieli Mbaga kwa kazi kubwa anayoifanya ya ukatili wa kijinsia.