Waziri wa Nishati Mh. January Makamba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhe. Peter Chibwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa ulinzi nchini Zambia, Mhe. Ambrose Lufuma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam.
**********
Na Beatrice SANGA- MAELEZO
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati imekutana na Serikali ya Zambia kujadili namna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli.
Akizungumza katika leo Desemba 6,2022 katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amesema kwa sasa inahitajika ulinzi zaidi katika bomba hilo ili kulinda usafirishwaji wa mafuta hayo na ndo maana wamekutana viongozi wa pande zote mbili ili kujadili usalama wa Bomba hilo.
“Kama tukisafirisha diseli maana yake usalama wa bomba unakuwa ni jambo kubwa kwa sababu inaweza kutokea kuchepushwa, hivyo sasa tukaamua serikali zetu mbili kufanya uratibu wa usalama wa hili bomba” Amesema Mhe. Makamba
Kwa upande wake Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhe. Peter Chibwe ameeleza kuwa hapo awali ambapo walikuwa wanasafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania kwenda Zambia ambako yanachakatwa gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa na serikali yao ilikuwa ikitumia ruzuku kubwa hivyo ni wakati sasa wamefanya mapinduzi kwa kusafirisha mafuta ambayo tayari yameshachakatwa.
“Ni wakati wa kufikiria ikiwezekana tuweze kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Tanzania kwenda Zambia hali itakayosaidia kupunguza ukataji miti ovyo kwa ajili ya mkaa na kuni na kuwezesha kutunza mazingirakatika nchi hizi mbili”. Amesema
Naye Waziri wa ulinzi Zambia, Mhe. Ambrose Lufuma ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa jambo hili pamoja na timu ya ufundi kwa kufanya kazi nzuri ndani ya siku mbili walizokaa ambapo wameweza kuja na mipango mbalimbali itakayotumika kulinda bomba hilo ikiwemo ufungaji wa camera za CCTV, matumizi ya drones na kuweka askari kwa ajili ya ulinzi masaa yote.