Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akitoa ufafanuzi wa michoro ya ramani ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akielekeza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firmin Msiangi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akisoma taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Wengine ni watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
*******************************
Na Happiness Shayo – Mwanza
Tarehe 28 Septemba, 2019
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameridhishwa na
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa kilichopo eneo la Pasiansi jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa
kituo hicho, Dkt. Mwanjelwa amesema ujenzi wa mradi huo uko
katika hatua nzuri hivyo, ameipongeza Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa kwa kufikia hatua hiyo.
“Hakika jengo hili ni la viwango, linaridhisha na vifaa vya ujenzi
vilivyotumika viko katika viwango bora” Mhe. Dkt. Mwanjelwa
amefafanua.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
kwa kutenga bajeti iliyowezesha ujenzi wa kituo hicho kwani mradi
huo ulianza tangu mwaka 2008.
“Matumizi ya mkandarasi na mshauri binafsi yalisababisha kuwapo
kwa gharama kubwa za ujenzi zilizosababisha kusimama kwa
ujenzi katika hatua za awali, lakini mwaka 2017/2018 Serikali ya
Awamu ya Tano ilithamini mradi na kutoa fedha zilizofanikisha
mradi kama unavyoonekana sasa” Mhe. Dkt. Mwanjelwa
amesisitiza.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na
Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amesema, Serikali iliamua
kujenga kituo hicho cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kwa
lengo la kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za ofisi za
serikali zilizopo kanda ya ziwa.
Bw. Msiangi amesema, kituo kitakapokamilika kitatumika kama
kituo mbadala cha kuhifadhi mifumo ya kumbukumbu na nyaraka
iliyopo katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu cha jijini Dodoma.
Naye, Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa
Mwanza, Bw. Victor Baltazar amemthibitishia Dkt. Mwanjelwa kuwa, ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi
Novemba, 2019.
“Mpaka sasa tumejenga jengo la utawala, maghala ya kuhifadhia
nyaraka kwa asilimia 95 na pia tumejenga uzio, eneo la kuegesha
magari, eneo la bustani, banda la walinzi na madereva kwa
asilimia 60” Bw. Baltazar amefafanua.
Ziara ya Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ya kutembelea kituo cha
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Mwanza ni sehemu ya
utekelezaji wa majukumu yake la kukagua utekelezaji wa miradi
iliyo chini ya Ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi wa umma nchini.