Waogeleaji wa Tanzania na viongozi mbalimbali wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa kanda ya tatu Afrika
Waogeleaji wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mashindano ya kanda ya tatu Afrika.
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya kanda ya tatu Afrika. Kamati iliyo ilipewa jukumu la kuandaa mashindano hayo chini ya Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA)
Dar es Salaam. Waogeleaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya wanaume na wanawake (Tanzanite) wameipeperusha vyema bendera ya nchi baada ya kushinda mashindano ya Kanda ya tatu Afrika yaliyofanyika hivi kariibuni kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana.
Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya nchi 10, waogeleaji wa Tanzania walikusanya jumla ya pointi 3,061 na kuzishinda nchi tisa katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa na kusisimua.
Tanzania ambayo iliwakilishwa na waogeleaji 63 pia ilikuwa nchi pekee iliyoshinda medali nyingi kushinda nchi zote zilizoshiriki katika mashindano hayo. Tanzania ilishinda jumla ya medali 110.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na chama cha mchezo huo cha kanda ya tatu Afrika, nafasi ya pili ilikwenda kwa Kenya ambayo ilijikusanyia pointi 2,768 na kufuatiwa na Uganda iliyojikusanyia pointi 2,521.50 na Zambia katika nafasi ya nne kwa kukusanya pointi 1,878.
Afrika Kusini ilishinda nafasi ya tano kwa kupata pointi 1,385. 50 ambapo Burundi ilishika nafasi ya sita kwa kupata pointi 653 na Sudan Kusini ikimaliza katika nafasi ya saba kwa kupata pointi 213.
Nchi za Djibouti ( pointi 87), Rwanda (pointi 67) na Ethiopia iliyopata pointi 47 zilimaliza katika nafasi ya nane, tisa na 10 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa naKilombero Sugar Company kupitia Bwana Sukari.
Wadhamini wengine ni JustFit, Kahawa Café, Spark rehabilitation, Gymkhana Club, International School of Tanganyika, FK International school, Hopac Hawks, Pepsi, Travelport, Azam, Stanmag Logistics, Wood Lab Décor, Burger 53, F&L Juice, G1 Security, Leo Club of Tanzania District 411C, Suraksha Team, Pyramid consumers, Four Points by Sheraron, Crown Hotel, Aura Suites na Protea Hotel Mariot- Courtyard.
Kwa upande wa medali, Tanzanian ilikusanya jumla ya medali za dhahabu 38, Fedha 38 na Shaba 34 ikifuatiwa na Kenya ambayo ilipata jumla ya medali 108 ambapo 46 ni dhahabu, Fedha 32 na Shaba 30.
Uganda ilipata jumla ya medali 85 ambapo 28 zilikuwa za dhahabu, 25 fedha na shaba 32 na Zambia ilipata jumla ya medali 56, 22 (dhahabu), 21 (fedha) na 13 shaba.
Afrika Kusini ilipata jumla ya medali 30 ambapo nane (8) ni dhahabu, nane za fedha na 14 za shaba. Nchi za Burundi, Sudan na Rwanda zilishika nafasi ya sita, saba na nane kwa kukusanua jumla ya medali 20, 10 na tatu (3) huku nchi za Ethiopia, Djibouti na Sudani Kusini zikiambulia patupu.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe aliwapongeza waogeleaji na timu zote shiriki kwa kufanikisha na Tanzania kuibuka washindi kwa mara ya tatu katika historia. Tanzania mara ya kwanza ilishinda taji hilo mwaka 2016 mjini Kigali, Rwanda na mwaka uliofuatia katika mashindano yaliyofanyika hapa nchini.
Shebe pia aliwapongeza wajumbe wa kamatiya maandalizi ya mashindanin hayo ambao ni Bella Faya, Geetha Prashant, Priscilla Zengeni, Lingesh Ramasamy, Martha Makoi, Opalina Nanyaro, Tunu Kinabo, Joan Laiser na Francisca Binamungu.