…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Singida
KATIBU Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko amekabidhi pampu 13 za umwagiliaji zinazotumia
nishati ya jua kwa vikundi 13 vya vijana
Vijana Halmashauri ya Manyoni, Itigi, Mkalama, Singida, Manispaa na
Iramba zenye thamani ya Sh.Milioni 23.4.
Akizungumza na vijana hao katika Ukumbi wa Ofisi za Shirika lisilo la
Kiserikali la SEMA mkoani hapa Mwaluko alisema mashine hizo zitawasidia
kuongeza kipato katika shughuli za kilimo cha bustani na kuwataka wazitunze ili
ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Aidha Mwaluko ametoa wito kwa vijana kuacha kulalamika kwamba hakuna ajira
na badala yake wajitume kufanya kazi za kilimo na ufugaji kwa kuwa bidhaa
zitokanazo na shughuli hizo zina soko kubwa ndani ya Mkoa na nje.
Aidha Katibu Tawala huyo amelishukuru Shirika la NSV (Nedhalend Development
Organization) kupitia Mradi wake wa OYE (Opportunities for youth Employment)
kwa msaada wa mashine hizo ambazo zimegharimu kiasi cha Milioni 1.8 kwa kila
moja ambapo shirika limechangia asilimia 68 na Kampuni iliyotengeneza
ikachangia asilimia 15 wakati vikundi vikachangia asilimia 17 ambao inalipwa
kwa miezi 16.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Usimamizi na Tathmini katika Mradi huo
wa OYE Belinda Masawe, amesema mashine hizo hutumia nishati ya jua ambayo
haitawaingizia gharama za uendeshaji Wanakikundi.
Hata hivyo Belinda ameendelea kufafanua kwamba mashine ina uwezo wa
kumwagilia shamba lenye ukumbwa wa ekari mbili kwa msimu mmoja na ina uwezo wa
kudumu kwa zaidi ya miaka kumi (10) ukipata mafunzo.
Aidha ameeleza kwamba vikundi hivyo vimepewa muda wa miaka miwili (2) wa
uangalizi na endapo zitaharibika kabla ya hapo vitarudishwa kwa muuzaji.
Akimalizia hotuba yake Belinda ameeleza kwamba mashine hizo zimetafutiwa
ubora wake na kubainika kwamba ni nzuri kwa mazingira kwa kuwa hazitoi moshi
wala mabaki ya mafuta ambayo yangechafua mazingira.
Awali akitoa maelezo ya ukaribisho Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida Fredrick
Ndahani, ameeleza kwamba fursa za biashara katika Mkoa huo nikubwa kwa kuwa
kuna miradi mingi imeanzishwa ikiwemo bomba la mafuta na miradi ya machimbo ya
madini kwamba ni soko kubwa.