Mwanza,
Uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) unapenda kuwatangazia wateja na umma kwa jumla kuwa safari za meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu zitasitishwa kwa muda wa wiki moja ili kupisha matengenezo madogo madogo (Services) yatakayofuatiwa na ukaguzi utakaofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ili kupata cheti cha ubora wa meli ambacho hutolewa kila mwaka.
Hivyo Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu haitafanya safari zake za kutoka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Kemondo na kutoka Bukoba kupitia Kemondo kwenda Mwanza kuanzia tarehe 27 November, 2022 hadi 04 Disemba, 2022.
MSCL inasisitiza kuwa utaratibu huu ni wa kawaida na hufanyika kila mwaka, pia unalenga kuendelea kutoa huduma bora inayozingatia usalama wa abiria na mizigo.
MSCL inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na;
Idara ya Masoko na Biashara