*******************
Kuelekea miaka ya Arobaini tokea kuanzishwa na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimetoa tuzo ya kuthamini Mchango mkubwa wa Mwanafunzi aliyewahi kuhitimu katika chuo hicho mnamo mwaka 2001, Dkt. Selemani Said Jafo ambaye alifanya vizuri katika masomo yake na kuleta tija na mchango mkubwa kwa Jamii tokea alipo hitimu masomo yake Chuoni hapo. Dkt. Jafo amekuwa miongoni mwa wanazuoni wachache sana walisoma SUA kupata tuzo ya aina hiyo kwa miaka tofauti tokea kuanzishwa kwa Chuo hicho.
Tuzo hiyo ameipata Dkt. Selemani Saidi Jafo kutokana na mchango wake mkubwa kwa jamii alio ufanikisha wakati alipokuwa anatimiza majukumu yake katika jamii kwa vipindi tofauti. Chuo cha Kilimo Sokoine kimekuwa kikifuatilia mwendendo na tabia za wanazuoni wao waliohitimu chuoni hapo ili kubaini mchango wao katika jamii.
Dkt. Selemani Saidi Jafo imebainika kwamba ameleta mchango mkubwa alipokuwa katika nafasi ya mtaalam wa kilimo wa Halmashauri ya Kisarawe kwa mwaka 2001 hadi 2005. Pia taarifa ya chuo hicho imeonyesha kwamba Dkt. Jafo alikuwa Mtanzania wa kuigwa kwa kuchapa kazi kwa kuleta matokea alipokuwa akifanyakazi katika shirika la Kimataifa la Plan International ofisi ya Tanzania kwa nafasi ya Meneja wa Miradi. Katika nafasi ya ubunge Dkt. Jafo amehudumia vyema wananchi wake sambamba na kuliwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la SADC ikiwa ni pamoja na kuwa Mweka hazina wa bunge hilo la SADC kwa matokeo chanya. Eneo lingine kubwa lililompa heshima hiyo ni kuwa kiongozi mwenye ari, mnyenyekevu, na anaye jituma kwa moyo mkubwa bila ya kuchoka kwaajili ya jamii alipokuwa waziri wa TAMISEMI na katika nafasi yake ya sasa ya waziri wa Muungano na Mazingira.
Wakati wa kupokea Tuzo hiyo Dkt. Selemani Jafo alisema “Hii ni heshima kubwa Sana kwangu, familia yangu, na taifa langu. Pia natoa Shukran za dhati kwa Uongozi Chuo kikuu cha Kilimo SUA Kwa kunipatia Tuzo hii kwa maana nilipata kusoma hapa miaka iliyopita katika ngazi ya Shahada na Wanafunzi wapo wengi Sana ila waliona wanipatie mie hasa kwa Mchango mkubwa nilioutoa katika nyanja mbalimbali katika jamii, alisema Dr Jafo”
Chuo kikuu cha Kilimo Sua leo 25.12.2022 kinahitisha Mahafali ya arobaini kwa kudahilisha wanafunzi katika kada mbalimbali ikiwemo ya Kilimo,Mifugo,Elimu na Afya.