Muhudumu wa huduma ya kwanza (RED CROSS) Mohamed Khamis Kombo akimpima shinikizo la damu Tatu Abass katika hafla ya Uzinduzi wa mpango wa uhamasishaji kuhusu shinikizo la damu huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya (hayupo pichani) wakati akizungumza katika uzinduzi wa Mpango wa uhamasishaji kuhusu shinikizo la damu (Healthy heart Africa) huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Dkt Salim Slim (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa shirika la Atrazeneca na kuimarisha afya Zanzibar (HIPZ) huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi wa kuimarisha afya Zanzibar Simon Kuhnert (HIPZ) akizungumza na wananchi na wahudumu wa afya kuhusu kujikinga na maradhi ya shinikizo la damu huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi kutoka Shirika la Atrazeneca Dkt Allan Mackenzie akizungumzia na wananchi kuhusu mikakati ya mradi wa mpango wa kutokomeza maradhi ya shindikizo la damu na kuimarisha afya za wananchi katika hafla ya Uzinduzi wa mpango wa uhamasishaji kuhusu shinikizo la damu huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Dkt Salim Slim akizungumza na wananchi wakati akizindua mpango wa uhamasishaji kuhusu shinikizo la damu(Healthy heart Africa) huko katika Kijiji cha Maafa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
PICHA NA RAHIMA MOHAMED HABARI MAELEZO