Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WATU wawili waliotambulika kwa jina la Ibrahim Juma na Mohamed Kibavu wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na kosa la kulawiti.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani ,Pius Lutumo alieleza hayo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kibaha.
Alisema hukumu hizo zimetokana na Jeshi hilo katika kushughulikia kesi za jinai, ambapo watuhumiwa hao walifanya matukio hayo ya ulawiti huko Bagamoyo na kufungwa kifungo cha maisha, kila mmoja katika hukumu iliyotolewa kwenye mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda Lutumo alifafanua, Polisi katika kushughulikia kesi za jinai kwa makosa makubwa na madogo kuanzia mwezi Octoba hadi Novemba mwaka huu ,kesi 80 zinazohusu jinai zikiwa na watuhumiwa 100 zilifunguliwa.
Hata hivyo, alieleza, kesi hizo ni pamoja na kubaka, kulawiti, unyang’anyi wa kutumia nguvu na wa silaha.
Kamanda Lutumo alisema ,kwa upande wa makosa madogo madogo kama shambulio watuhumiwa nane walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa miezi sita hadi 12 jela huku watuhumiwa 14 wa wizi wakihukumiwa mwaka mmoja jela.
Vilevile, Jeshi hilo katika kupambana na wahamiaji haramu watuhumiwa wanne raia wa Tanzania walikamatwa kwa kusafirisha wahamiaji haramu.