Na Oscar Assenga,TANGA. MAMLAKA ya Mapato Tanzania Mkoani Tanga (TRA) leo wamekutana na kuzungumza na walipa kodi Mkoani Tanga katika halfa iliyokwenda sambamba na kuwapongeza kwa ulipaji kodi wao wa mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao uliiwezesha kuvuka lengo na kuibuka kidedea katika mikoa yota nchini. Halfa hiyo ilikwenda sambamba na kuwatembelea wateja wakubwa mkoani Tanga ikiwemo wafanyabiashara katika eneo la barabara ya 14 Jijini Tanga na Kiwanda cha PPTL ambako walizungumza nao. Akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kwamba mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inakusudia kukusanya kodi kiasi cha shilingi Billioni 232.69 ikiwa ni malengo ya serikali sawa na ongezeko la asilimia 37 ya mwaka wa fedha uliopita. Alisema kutokana na uwepo wa Kutokana na ongezeko hilo alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara mkoa humo kuendelea kushirikiana kikamilifu na mamlaka ya mapato katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na kwa hiari ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya kuendelea kung’ara katika ukusanyaji wa kodi hapa nchini Meneja huyo alisema mamlaka hiyo kuibuka kidedea ni kutokana na walipa kodi wa mkoa wa Tanga kulipa kodi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 . Alisema kwa mkoa wa Tanga walikuwa wamepangiwa lengo la kukusanya billion 169.68 lakini wao wameweza kukusanya billioni 207.52 ikiwa ni sawa na asilimia 121.6% hivyo waliwashukuru kwa kuwawezesha kufikia lengo hilo. Meneja huyo alisema pia katika mwaka wa fedha 2022/2023 lengo lao la ukusanyaji limeongezeka na kufikia bilion 63 ambayo ni sawa la ongezeko la asilimia 37% ya lengo la mwaka huu ni bilion 232.69 kwa hiyo wana kazi kubwa ya kufanya. Alisema kwa sababu mwaka uliopita waliweza hatua ambayo imepelekea mwaka huu wameongezewa lakini katika hayo yote hatukuweza pekee yetu bali ni ushirikiano wenu wadau na hivyo kuweza kulipa kodi kwa hiari Hata hivyo Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara katika mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kulipa kodi pamoja na kutekeleza maagizo ya serikali ya kulipa kodi kupitia mfumo wa kielektroniki. “Lakini pia niwatake kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato pale panapotokea changamoto yoyote ikiwemo ya kusitisha biashara au kuhama”alisema Awali akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini Selestini Kiria aliipongeza mamalaka hiyo kwa mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa fedha uliopita. Sambamba na hilo pia amewaomba kuendelea kuboresha huduma zao ili kuzidi kuwavutia wateja kuweza kulipa kodi kwa wakati. Akizungumza wakati alipotembelewa kwenye duka lake Mfanyabiashara Wilbard Mallya aliipongeza mamlaka hiyo kwa huku akiiomba Serikali kuwaangalia wafanyabiashara kwenye suala la kodi pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma. |