Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akiwa na Manejimenti ya UDOM muda mfupi baada ya kuwasili chuoni hapo kwa mazungumzo na Menejimenti ya Chuo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Jeremy Kusiluka (kushoto), Naibu Makamu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii Prof. Razack Bakari Lokina (katikati) na Naibu Makamu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson Saria (haonekani pichani)
…………………………..
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo tarehe 24 Novemba 2022 amefika chuoni hapo na kufanya mazungumzo na Menejimenti.
Akiwa chuoni hapo pamoja na masuala mengine Dkt. Tax amepokea taarifa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya shughuli mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika chuoni hapo katika kipindi cha mwisho wa mwaka huu 2022. Taarifa hiyo ilihusisha maendeleo ya maandalizi ya Sherehe ya Mahafali ya 13 ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika tarehe 1 na 2 Novemba 2022, na kufanyika kwa Mkutano wa Wanazuoni wa Chuo hicho.
Akizungumza muda mfupi baada ya Dkt. Tax kuwasili chuoni hapo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Jeremy Kusiluka ameeleza kuwa ni utaratibu wa kawaida wa utendaji wa Menejimenti kutoa taarifa kwa Mkuu wa Chuo kila mara kuhusu maendeleo ya shughuli mbalimbali zinazoendelea Chuoni hapo.
Mhe. Waziri Dkt. Tax aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Juni 2021.