Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji NICOL, Dk. Gideon Kaunda akizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa nane uliofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salam Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji NICOL wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa kwenye mkutano mkuu wa nane wa kampuni hiyo uliofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wanahisa wa kampuni ya uwekezaji NICOL, akichangia jambo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ulipitisha gawio la Sh 20 kwa kila hisa Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji NICOL, Dk. Gideon Kaunda akizungumza na wanahisa wa kampuni hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa nane uliofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salam
*********************
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Uwekezaji ya NICOL imepata faida ya shilingi bilioni nne na imepitisha gawio la Sh bilioni 1.2 kwa wanahisa wake litakalotolewa mwezi ujao.
Gawio hilo lilipitishwa siku ya Jumamosi katika maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa mwaka wa wanahisa uliofanyika kwa njia ya video kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Akizungumza mara baada ya mkutano huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NICOL, Erasto Ngamilaga, alisema Mkutano Mkuu ambao umefanyika ni takwa la kisheria kwa makampuni kama hayo kufanya na wanahisa wake wote.
Alisema kwenye mkutano huo wamehudhuria wanahisa wa mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam ambapo wale wa mikoani walifuatilia mkutano huo kupitia mtandao.
Alisema kwenye mkutano huo wamepata fursa ya kuwaeleza wanahisa namna kampuni ilivyopata faida ya Sh bilioni nne kabla ya kodi na Sh bilioni 3.8 baada ya kodi.
Alisema wanahisa wamepitisha gawio la Sh 20 kwa kila hisa ambayo itaanza kulipwa 15.12.200 na kwamba ni ongezeko la gawio la Sh 17 ambalo lilishalipwa kwenye mahesabu ya mwaka 2021.
“Wanahisa wamefurahi sana kuona kampuni inafanya vizuri na sisi viongozi tumewaaahidi kuweka mikakati mizuri zaidi kuhakikisha kampuni inazidi kusonga mbele na kupata faida kubwa zaidi siku za usoni,” alisema Ngamilaga
Mwenyekiti wa Bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda, alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa gawio kila mwaka na aliishukuru bodi mpya kwa kuwekeza sehemu mbalimbali hasa kwenye hati fungani za serikali.
Alisema kampuni hiyo imewekeza asilimia 30 ya uwekezaji wake kwenye hati fungani na ndiyo sababu kampuni hiyo imeendelea kupata faida mwaka hadi mwaka na kuwapa gawio zuri wanahisa wake .
Alisema wanahisa wa NICOL nchi nzima wanafikia 30,000 na wamesambaza sehemu za mikutano ili kuwafikia wanachama wengi badala ya kulazimika kuja Dar es Salaam kwenye mKutano Mkuu wa mwaka.
“NICOL inapenda kuona wanahisa wake wanapata gawio kila mwaka na kweli kampuni imefanya vizuri na gawio limeongezeka kutoka Sh 17 na sasa tutalipa sh 20 kiwango ambacho kampuni zingine zimeshindwa kufikia na tunadhani mwakani tutazidi kuongez gawio kubwa zaidi kwa wanahisa wetu,” alisema
Mwanahisa Mutamwega Mugaywa, alisema anashukuru kuona kampuni ya NICOL imesimama na kuonyesha matumaini makubwa kwa wanahisa wake.
“Nifuraha kubwa kuona NICOL inabeba uchumi na nawashauri watu wengine waje wanunue hisa zao mapema NICOL kwasababu kuna faida nyingi kuwa mwanahisa wakampuni ya wazalendo,”
“Nawapongeza viongozi kwa kusimamia vizuri Kampuni na sasa tunapata gawio zuri nawashauri wengine nao wachangamkie hisa za kampuni yetu,” alisema
Mwanahisa mwingine, Suzana Masele alimongeza Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Dk. Gieon Kaunda kutokana na anavoisimamia kampuni hiyo na menejimenti nzima.
“Nampongeza kwani anavyoisimamia vizuri kamouni utadhani ni kampuni yake binafsi ukiangalia ilipokuwa huko nyuma ilikuwa kama imekufa lakini mwenyekiti wa sasa anajua anachofanya na tunaelekea pazuri zaidi,” alisema