Bishop Dr Suleiman Elisha Mjumbe na katibu wa Bodi (TWWT) kushoto akimkabidhi cheti Dr Nathanael Kigwila Kulia kwake, Kushoto kwa ni Mke wa Kigwila Bi Gloria Kigwila pamoja na mtoto wao Enock Kigwila. Octavian Mutayoba Katibu Mtendaji TWWT, kulia, akimkabidhi Dr Nathanael Kigwila kofia pamoja na Tshirt kwa ajili ajili ya ubalazo wa Taasisi hio nchini Marekani
****************************
Mwakilishi wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bishop Dr Suleman Elisha leo hii amemtunuku Bishop Dr Nathanael Kigwila cheti cha heshima kutambua mchango wake kwa taifa kama mtanzania anayeishi Nchini marekani cheti hicho kimetolewa katika hafla za kuhitimisha mafunzo ya kiroho na uzalendo yaliyofanyika kwa takribani siku nne katika ukumbi wa kanisa la The Growing Mission Church (GMC) lililopo Mapinga Pwani.
Halfa hio imeuzuiliwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya TWWT akiongoza Dr Ezekiel Kyogo ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya wananchi wazalendo na mratibu msaidizi wa polisi makao makuu ya polisi Dodoma Octavian Mutayoba katibu mtendaji TWWT na Ayubu Musa afisa mahusiano wa TWWT.
Taasisi ya Wananchi Wazalendo Tanzania (TWWT) imemtunukia Bishop Nathaniel Kigwila Mtanzania anayeishi Nchini Marekani kwa kutambua kazi mbalimbali ambazo amekuwa akizifanya nchini pamoja na kukaribisha wawekezaji kutoka nchini Marekani .
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo Dr Ezekiel Kyogo amesema ni watanzania wachache wanaoishi nchi za nje na wanakumbuka kuwekeza nyumbani nchini Tanzania kama alivyofanya Dr Nathanael Kigwila, kutokana na mchango wake huo taasisi hiyo pia imemteua Bishop Kigwila kuwa balozi wa Taasisi hiyo nchini Marekani ili kuendelea kuhamasisha uzalendo na kuipenda Tanzania.
Dr Nathanael Kigwila ameishi nchini marekani kwa Zaidi ya miaka 30 na katika kipindi hiko amefanikiwa kupeleka Zaidi ya watanzania 2000 kupata mafunzo mbalimbali, Pamoja na kupeleka wanafunzi hao Nchini Marekani pia Bishop Kigwila amefanikiwa kuleta wawekezaki ambao wamewekeza katika Dawa za binadamu kwa kujenga viwanda katika mkoa wa Pwani pamoja na kupeleka dawa hizo katika jeshi la Zanzibar KMKM, Uwekezaji wa kilimo cha viungo unaoendelea katika kijiji cha Mkange Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Pwani uliojiri Zaidi ya watanzaia 50 pia Kiwanda cha kusaga unga kilichopo eneo la mlingotini Mkoani Pwani, sambamba na hayo Dr Nathanael Kigwila anahudumia Zaidi ya watoto yatima 150 wakishirikiana na wawekezaji na makanisa kutoka nchini Amerika.
Tunamshukuru Mungu alieyetufanikisha kufanya hivyo, kila mtu ana kitu na kusudi la kufanya ambalo Mungu ameliweka katika maisha yetu, tutaendelea kujitahidi kutumia nguvu na nafasi ambazo Mungu ametupa kuendelea kusaidia watu wengi Zaidi ameongea Bishop Nathanael baada ya hafla hiyo.
Bishop Dr Nathanael Kigwila ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la GMC ndiye aliyeratibu mafunzo hayo ya kiroho kwa viongozi mbalimbali wa makanisa kutoka katika madhehebu mbalimbali. Mafunzo hayo yalidumu kwa siku 4 yaliongozwa na wakufunzi mbalimbali kutoka nchini Tanzania, Kenya na Marekani.
Wakufunzi hao ni pamoja na Mwinjilisti Terry L Anderson, Jonathan Yergin, Anne Yergin and Trent Radbil kutoka kanisa la Wildwood Baptist lililopo Jimbo la Atlanta nchini Marekani, wakufunzi wengine ni Dr Anne Kiteme kutoka Kenya, Bishop Deo Lubala na Bishop Charles Gadi, Pamoja na Dr Ezekiel Kyogo.
Wakufunzi hao wamefundisha mambo mengi yanayohusu uongozi wa viongozi wa kiroho katika kuhamasisha jamii kupata mabadiliko chanja, pamoja na mafundisho hayo Dr Ezekiel Kyogo amefundisha somo la uzalendo kwa kipindi chote cha mafunzo na kumtaja Dr Nathanael Kigwila kama mfano wa kuigwa na watanzania wengi kwa kuipenda na kuitangaza nchi yake.
Obedi Mwakipiti mshiriki na mwimbaji katika mafunzo hayo amewasifu wakufunzi hao kutoka nchi mbalimbali na kusema wameongeza kitu kikubwa sana katika maisha yake, amejifunza namna sahiihi ya kusoma na kuielewa biblia pamoja na namna nzuri ya kuishi na watu wenye mitazamo ya Imani tofauti.
Kwa upande mwengine, Jackline Lukosya Mshiriki katika mafunzo hayo amejifunza mambo mengi yakiwemo malezi ya familia hasa kushirikiana kati ya baba na mama somo lililofundishwa na Dr Ezekiel Kyogo pamoja na hayo amemsifu Dr Nathanael Kigwila kuwa kuwa mpambanaji katika masuala ya kiroho na katika uwekezaji nchini Tanzania.
Dr Nathanael Kigwila ametoa wito kwa watanzania waliopo nje ya nchi kuendelea kukumbuka nyumbani na Zaidi kuendelea kuwekeza nchini Tanzania, pia Dr Kigwila ameiomba serikali kufanikisha suala la Uraia pacha ambao utamuwezesha mtanzania aneyeishi nje ya nchi kufanya mambo Mengi.