Katika picha ni Banio linalopokea maji kutoka katika Bwawa la Umwagiliaji Ulianyama Wilayani Sikonge na kupeleka maji katika mfereji na mashamba ya kilimo cha Umwagiliaji katika Skimu hiyo.
Bwala linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji Uliyanyama lenye mita za ujazo milioni mbili.
Katika picha ni moja ya miundombinu iliyojengwa kiufanisi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Uliyanjama iliyopo Wilayani Sikonge Mkoani Tabora ili kuweza kumudu kasi ya maji yanayoingia katika mashamba na kuzuwia upotevu wa maji na mmomonyoko wa ardhi.
Katika Picha ni magunia ya mpunga katika moja ya ghala la kuhifadhia nafaka lililojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kayika skimu ya ka Kilimo cha Umwagiliaji Uliyanyama Mkoani Tabora.
Bw. Simon Kalosa katibu wa chama cha umwagliaji cha Uliyanyama Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, akiongea kuhusu mafanikio yaliyopatika katika skimu hiyo baada ya Uboreshaji wa Miundombinu ya umwagiliaji.
………………..
Na; Mwandishi Maalum – Sikonge Tabora
Wakulima wa kilimo cha Umwagiliaji katika Skimu ya Kilimo cha Umwagililiaji ya Uliyanyama Iliyopo Wilayani Sikonge Mkoani Tabora waiomba Serikali kuwasaidia kupata Mikopo kupitia taasisi za kibenki hususan Bank ya kilimo ili kuweza kuwasiaidia kutatua changamoto ya zana za kilimo pamoja na Pembejeo.
Akiongea na wataalam na wanahabari kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mwenyekiti wa Umoja wa Umwagiliaji katika skimu hiyo Bw.Dickson Masungwi amesema kuwa wakulima wakipatiwa mikopo wanaweza kujikwamua katika shughuli zao za kilimo na kupanua kiwango cha uzalishaji kwa maana watalima kwa wakati muafakana wataweka mbolea kwa muda mzuri na kuongeza uzalishaji.
‘Sisi kama wakulima tukipata mikopo hata kwa kupitia umoja wetu huu tunaweza kujikwamua kwa kununua zana za kilimo kama vile ma trekta ya kulimia na kuvunia mpunga.’ Alisema Bw. Masungwi.
Aidha Bw. Masungwi aliendelea kuiomba Serikali ya Awamu ya tano kuwakumb uka wakulima kwa kuwapatia Pembejeo za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kuwaongezea watalam watakokuja na mbinu mpya za kisasa katika eneo la umwagiliaji ili kuweza kuongeza tija katika kilimo hicho.
Sambamba na hilo wakulima katika skimu hiyo wameomba kufanyika kwa upanuzi wa eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa kwa hekta 200, kuongezwa kwa kina cha bwawa la umwagiliaji na kuinua tuta ili kuweza kusaidia upotevu wa maji wakati wa masika na kusadia katika msimu wa pili wa kilimo ambao ni wkati wa kiangazi.
Skimu ya Umwagiliaji Uliyanyama ina ukubwa wa eneo la Hekta 400 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, ambapo hekta 200 zimeshaendelezwa na hekta 122.4 ndizo zinazomwagiliwa.