Majadiliano yakiendelea katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 chuoni hapo ambapo mgeni rasmi akiwa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga.Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga akifuatilia Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa William Anangisye akizungumza jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga akizungumza katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Mwenyekiti wa Baraza, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akizungumza katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Profesa Bonaventure Rutinwa akizungumza katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utafiti, Profesa Bernadeta Killian akizungumza katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam zilizofanyika leo Novemba 10,2022
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kwa kuzingatia Changamoto zinazoibukia katika jamii,Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kimekuwa cha mfano katika tafiti na huduma kwa jamii kwani kimekuwa kikitenga bajeti ya ndani katika kuwezesha shughuli za utafiti ambazo zimekuwa zinaleta manufaa makubwa kwenye jamii.
Ameyasema hayo leo Novemba 10,2022 Jijini Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof.Florens Luoga, katika Sherehe za Kufunga Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetoa mchango mkubwa katika Taifa kwa kuwa kitovu cha utafiti, ufundishaji na ujifunzaji, Wahitimu wengi wameajiriwa Serikalini, katika sekta binafsi, na katika mashirika ya Kimataifa.
“Imani kubwa ya Serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kimataifa kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni kubwa na inatokana na ubora wa wahitimu katika kufikiri, kuchanganua mambo, na kutatua changamoto mbalimbali katika vituo vya kazi, jamii, na Taifa kwa ujumla”. Amesema
Amesema ukuaji wa taasisi hiyo unadhihirishwa na ongezeko kubwa la uwezo wake kudahili kutoka wanafunzi 14 wa sheria mwaka 1961 hadi kufikia idadi ya sasa ya Elfu Arobaini na Mbili (42,000).
“Huu ni mchango mkubwa kwa jamii yenye uhitaji mkubwa wa fursa za elimu ya juu. Nafahamu kwamba hatua hii inakwenda sambamba na ongezeko la rasilimali watu ambapo kwa sasa chuo kina idadi ya watumishi wapatao 2,435”. Amesema
Aidha amesema Miaka 60 ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam inakwenda sambamba pia na matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo kutoa kutumia wataalam wa ndani katika kutengeneza mfumo wa kisasa wa usimamizi wa udahili, kanzudata ya wanafunzi na matokeo.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Anangisye amesema walikuwa na shughuli za maadhimisho hayoo kwa mwaka mzima yaani kuanzia tarehe 25 Oktoba 2021 Chuo kilipotimiza miaka 60 ya kuanzishwa kwake hadi leo hii kinapohitimisha maadhimisho hay.
“Tulifanya hivi makusudi kwa kuzingatia uzito wa maadhimisho yenyewe. Tulifahamu tusingetenda haki kwa Chuo chetu kwa kutenga siku moja peke yake kuadhimisha miaka 60”. Amesema Prof.Anangisye.