Mume wa Mnufaika wa TASAF Hawa Diwani, Abdallah Lukange Lukange ambao wanafanya kilimo cha mbogamboga na mpunga akielezea mafanikio waliyonayo baada ya kupata ruzuku ya uzalishaji kutoka TASAF. |
Na Dotto Mwaibale, Bagamoyo, Pwani.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa mwaka wa fedha 2022/
2023 imepokea zaidi ya Sh. 1 Bilioni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wilayani humo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Shauri
Selenda,alisema hayo juzi kwa waandishi wa habari na timu ya maafisa wa TASAF
waliokuwa kwenye ziara ya kuwatembelea walengwa
kuona kazi mbalimbali wanazozifanya baada ya kuwezeshwa .
Alisema katika fedha hizo Sh.1.76 Bilioni walizipokea kwa ajili ya ruzuku
ya uzalishaji na Sh.512 Milioni walipokea
kwa ajili ya ruzuku za kawaida na kuwa ruzuku za uzalishaji zinakwenda
kusaidia kwenye shughuli za kilimo, ufugaji na biashara ndogondogo.
Alisema kwa fedha za ruzuku ya kawaida zinakwenda kusaidia kwenye maeneo
mengine kama ya uvuvi na ufugaji lakini hizo milioni 620 kwa ajili ya ruzuku za
uzalishaji zinakwenda kuwanufaisha
walengwa 1320 ambapo kati yao waliopata ruzuku za uzalishaji ni walengwa
1158 sawa na asilimia 88.
Selenda alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo na
mchango mkubwa inaoutoa kwa wilaya hiyo na kuwa wao kama viongozi wajibu wao ni
kusimamia na kuona wananchi wanaikuza mitaji yao kwa ajili ya kupata maendeleo.
Mratibu wa TASAF Wilaya ya Bagamoyo, Rose Mndeme alisema wilaya hiyo ina
jumla ya kata 11 na kuwa vijiji 26 vipo kwenye mradi wa TASAF vyenye walengwa
3056 ambao wanalipwa ruzuku za aina tatu, ruzukuya kawaida, kufanya kazi kwa
miradi (ajira ya muda mfupi) na ruzuku ya uzalishaji.
Alisema katika ruzuku ya uzalishaji wanawalengwa 1320 ambao wamepewa ruzuku
ya Sh.620 Milioni kwa ajili ya kwenda kutekeleza miradi ya ufugaji wa mbuzi ,
kuku, ng’ombe, kilimo cha mbogamboga, ukaangaji wa samaki na kuziuza, biashara
ndogondogo kama za kuuza madera, usukaji wa mikeka na nyinginezo.
Alisema ili kusimamia walengwa hao waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa
kuna timu ya wawezeshaji 26 kutoka katika kata hizo 11kutoka katika idara za
mifugo, maendeleo ya jamii,kilimo na afya ambao wanawatembelea waengwa hao 1320
ili kujua maendeleo yao na changamoto ambazo wanazitafutia ufumbuzi.
“Kufuatia timu hiyo abayo inakwenda kutoa ushauri wa kitaalamu katika
wilaya yetu miradi yote inayofanywa na walengwa inakwenda vizuri tunashukuru
Mungu hivyo tunategemea kuwatoa kwenye mpango ili waweze kuwapisha watu wengine
kwa kuwa sasa wameweza kusimama wenyewe” alisema Mndeme.
Mndeme alitumia nafasi hiyo kumshuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo Shauri Selenda, Mkuu wa Wilaya, Zainab Abdallah kwa usimamiaji mzuri wa
miradi hiyo pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi na
kuzielekeza kuwasaidia watanzania wa maisha ya chini ili waweze kujikomboa
kiuchumi.
Afisa Ufuatiliaji wa Miradi TASAF, Janeth Mtelelah alisema fedha zote
zinazotolewa kwa walengwa zinatolewa kwa njia ya mitandao ya simu na njia ya
benki ambapo walisaidiwa kufungua
akaunti zao na kupata fedha zao pasipokuwa na changamotozozote.
Baadhi ya walengwa waliotembelewa na miradi yao kukaguliwa ni Hidaya
Mnyamisi mkazi wa Magomeni Bagamoyo ambaye ni mfugaji wa kuku, Zulfa
Emmanuel ambaye anauza samaki wa
kukaanga, Sikuzani Bwana ambaye
aanafanya biashara ndogondogoya genge, Halima Juma, ambaye ni mkulima na anauza
samaki, Hawa Diwani ambaye anasaidiwa na mume wake Abdallah Lukange ambao
wanafanya kilimo cha mbogamboga na mpunga.
Wengine ni Mwanaheri Dalu ambaye ni mshonaji wa nguo na Elizabeth Stephano
ambaye anajishughulisha na biashara ya duka.