Afisa habari kutoka tume ya maadili ya viongozi Serikalini Halima Jumbe Said akiwasilisha mada ya maadili kwa masheha na madiwani ( hawapo pichani) wa Wilaya ya Mjini wakati akitoa mafunzo ya maadili katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba. Masheha na madiwani kutoka wilaya ya Mjini wakiwasikiliza kwa umakini wakufunzi kutoka tume ya Utumishi Serikalini wakati wakipatiwa mafunzo ya maadili katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba.
Afisa usajili kutoka tume ya maadili ya viongozi Abdulatif Ali akiwasilisha mada kuhusu mgongano wa kimasilahi kwa masheha na madiwani wa Wilaya ya Mjini wakati akitoa mafunzo katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba. Baadhi ya masheha wakiuliza maswali kwa maafisa kutoka tume ya maadili ya viongozi huko katika ukumbi wa skuli ya sekondari Lumumba.
PICHA NA RAHIMA MOHAMED HABARI MAELEZO.
**********************
Na Bahati Habibu Maelezo 7/11/2022
Viongozi na watumishi wa Umma wametakiwa kufuata misingi na maadili ya Umma ili kuleta maendeleo na kuimarisha utawala bora nchini.
Akitoa mafunzo ya Maadili ya Uongozi kwa masheha na madiwani wa Wilaya ya Mjini Unguja huko katika ukumbi wa skuli ya Lumumba, Afisa Usajili kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar Abdulatif Ali amesema kufuata misingi na maadili ya umma yana yanapelekea kuwepo uwajibikaji mzuri na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu katika jamii
Amesema maadilii kwa viongozi na watumishi wa umma hujenga uaminifu na utendaji kazi kiufanisi kwa kuimarisha utawala bora na kuleta maendeleo kwa kukuza wa nchi
Afisa huyo ameleza lengo la mafunzo hayo ni kuwaweka viongozi na watumishi wa umma kufuata misingi na maadili umma na kutokuvunja sheria ya maadili ya umma ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji.
“Mgongano wa maslahi ni miongoni mwa matatizo yanayorejesha nyuma maendeleo ya nchi na kuhakikisha wanafanya majukumu yao bila ya upendeleo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na tume hiyo”, amefahamisha Afisa huyo.
Nae Afisa Habari wa Tume Halima Jumbe Said amewasisitiza viongozi hao kuyatumia mafunzo ya maadili ya umma ili kuwa viongozi bora na kuleta maendeleo ya nchi.
Amewataka viongozi hao kuzitumia vyema nyadhifa zao walizopewa katika kuwatunikia wananchi na kuacha tabia ya kujipatia maslahi binafsi kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.
Nao masheha hao wameiomba tume ya Maadili kuwapatia viongozi wa umma mwongozo wa Sheria utakaowasaidia katika kutekeleza majukumu kwa uweledi.