……………………
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutoa pole kwa Waarhirika wote wa ajali ya Ndege ya Shirika la Precision Air ili iliyotokea huko Bukoba Mkoani Kagera.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya Ndege ya Shirika la Precision Air iliyotokea leo katika Ziwa Victoria Bukoba. Naungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa waathirika wote wa ajali hii. Nawashukuru wote wanaoendelea kushiriki katika zoezi la uokoaji, Tuzidi kumwomba Mungu atupe subira katika wakati huu mgumu”. Aliandika Waziri Balozi Dkt. Chana, katika ukurasa wake wa Twitter.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa, idadi ya waliopoteza maisha ni 19 katika ajali hiyo iliyotokea Leo asubuhi kwenye Ziwa Victoria na manusura 26.