Ng’ombe wakinywa maji katika eneo la Mnazi kwenye mto Ruaha ambayo ni sehemu ya hifadhi ya Ruaha,Mbarali wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mbegu za zikiwa zimewekwa kwenye moja ya shamba katika eneo Mnazi lililopo katika Hifadhi ya Ruaha lililopo Mbarali mkoani Mbeya.
Maji yakiwa yamechotwa na wananchi walioko katika eneo la Hifadhi ya Ruaha eneo la Mnazi wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mkazi katika Hifadhi ya Ruaha katika eneo la Mnazi Pawa Shigela akizungumza kuhusiana na uwepo katika hilo na kuwa sio sehemu ya hifadhi.
Mkazi wa katika hifadhi ya Ruaha katika eneo Mnazi Simon Matonya akizungumza juu ya uhalali wa kuwepo katika eneo la hifadhi kwa kudai eneo hilo sio sehemu ya hifadhi.
*********************
*Matuta makubwa yawekwa kuzuia maji kutiririka kwenye mto.
Na Mwandishi Wetu
Mashamba makubwa yaliyo katika Hifadhi ya Ruaha katika eneo Mnazi ndio chanzo cha kukauka kwa mto Ruaha.
Mashamba hayo yako katika hifadhi kutokana na Tangazo la Serikali 28 maarufu GN 28 ambapo wananchi walivamia na kuendesha kilimo na ufugaji na kusababisha mto Ruaha kutokuwa na mririko wa maji.
Mashamba ya Mnazi yamewekwa kingo kubwa kuzuia maji yasiingie mto Ruaha na wakati mwingine wanachukua maji Mto kwa mashine za kusukuma maji.
Kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya Mto Ruaha Kituo cha Wanahabari,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA)wamefika katika eneo la Mnazi kuona shughuli za kilimo na ufugaji zilivyoathiri mto Ruaha .
Akizungumza mmoja ya wananchi waliokutwa kwenye mashamba ambayo ni hifadhi Pawa Shigela amesema kuwa wenyewe wamezaliwa hapo na kusema sio hifadhi kwa kudai hifadhi iko mbele.
Amesema kuwa kama watakiwa kuondoka watawasikiliza wazazi wao juu ya kuondoka na watakapoambiwa wataondoka kwenye hifadhi hiyo.
Mkazi katika hifadhi ya Ruaha kwa eneo la Mnazi Simon Matonya amesema kuwa hata hawaelewi kuhusu eneo hilo kuwa ni hifadhi na kama serikali itasema waondoke wataondoka kwani hawatabishia agizo la serikali.
“Sisi tumezaliwa hapa hatujui sehemu ya hifadhi ninachojua hifadhi iko mbele yetu lakini sasa hatuwezi kuibishia serikali lakini tunakwenda wapi”amesema Matonya.
Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi ‘Afande Sele’ amesema kuwa kwa ukubwa wa mashamba ya Mnazi kamwe Mto Ruaha hauwezi kutirisha maji.
Amesema ukame uliopo sasa katika mto Ruaha ni madhara makubwa katika nchi hali ambayo umefika wakati wa kuchukua hatua kwa jamii juu ya kulinda mazingira.
Aidha amesema kuwa makundi ya Ng’ombe yaliyo katika mto Ruaha ndio yameongeza ukame na kufanya baadhi ya wanyama kufa.