Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida kupitia namba 15089 uliofanyika katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama leo Novemba 5,2022
Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB wakifurahia pamoja wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS shortcode) kupitia namba 15089
**
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS shortcode) kupitia namba 15089 ili kuboresha zaidi huduma zake za Kibenki.
Mfumo wa kupokea maoni ya wateja kwa njia ya SMS umezinduliwa leo Jumamosi Novemba 5,2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ukihudhuriwa pia na wateja na Mameneja wa matawi ya Benki ya CRDB yapatayo 26 katika Kanda ya Magharibi inayoundwa na mikoa ya Shinyanga , Tabora , Kigoma , Geita na wilaya ya Segerema na Buchosa.
Mfumo huo ni rahisi sana kwani wateja wake hawatahitaji kutumia intaneti katika simu ya kiganjani ikiwa ni huduma mpya na ya kwanza kutumiwa na Benki ya CRDB hapa nchini pamoja na Afrika na Mashariki na kati na Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza kutumia kupokea maoni ya wateja kwa kutumia SMS ya kawaida (Normal SMS) kwa namba 15089.
Akizindua mfumo huo, Mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga ameipongeza benki ya CRDB kwa kwenda na kasi ya dunia katika mifumo ya matumizi ya kidigitali sasa kupitia njia hiyo wateja watatoa maoni yao popote pale na kwa simu za kawaida .
“Njia hii mpya tuliyozindua leo ya kutuma ujumbe mfupi wa (SMS) ni rafiki na rahisi kwani mteja hataihitaji kuwa na gharama ya kutumia intaneti kwenye simu yake wala simu janja na anaweza kutumia mtandao wowote”,amesema Kiswaga.
“Nitoe wito kwa benki ya CRDB ni mzidi kuongeza juhudi katika kutoa huduma bora ili muendelee kuwa mfano wa mafanikio kwa taasisi za wazalendo na ninawahakikishia Serikali ipo nanyi bega kwa bega hivyo kwa pamoja tufanye kazi ya kuijenga nchi yetu” amesema Kiswaga.
Akieleza mfumo huo Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Jumanne Wagana amesema kwa Afrika Benki ya CRDB itakuwa ya kwanza kutumia mfumo huo ambapo mteja atatuma SMSkwa kutumia simu yoyote na bila intaneti.
Naye Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa benki ya CRDB , Yolanda Uriyo amesema matumizi ya mfumo yanalenga kuboresha mifumo ya huduma kwa wateja ya utoaji wa maoni .
Uriyo amesema awali mteja akitaka kutoa maoni ilikuwa kwanza lazima uwe na simu janja yenye kutumia intaneti kwa sasa wateja wanapotaka kutoa maoni, watatoa maoni yao kupitia njia ya SMS kwa simu za kawaida na kwa gharama nafuu.
Amesema benki ya CRDB tayari imezindua mfumo huo, Visiwani Zanzibar kwa mikoa yote ya Pwani lengo ni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja ambao sasa anayetoa maoni atatuma akiwa popote pale hata nyumbani.
Kwa upande wao wateja wa benki hiyo waliokuwa wamehudhuria uzinduzi wa mfumo huo wameipongeza benki ya CRDB kwa kuendelea kuwajali wateja wake na sasa watatoa maoni kwa SMS.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Jumanne Wagana akitoa ufafanuzi mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida (SMS shortcode) kupitia namba 15089
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Benki ya Yolanda Uriyo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kupokea maoni ya wateja wa Benki ya CRDB kwa njia ya meseji za kawaida kupitia namba 15089
Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB wakifurahia pamoja