*********************************
Na Silvia Mchurua;
Kagera;
Serikali kupitia wizara ya ujenzi imewataka wakandarasi wazawa kuhakikisha wanatekeleza miradi ya barabara kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kujiepusha uhujumu.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa ujenzi Elias Kuandikwa wakati akizungumza na wakandarasi wanaojenga barabara za muhutwe kamachumu, kanyambogo rubya na muleba Kanyambogo zilizopo wilaya muleba.
Amesema kuwa endapo wakandarasi hao wataendelea kutekeleza miradi ya serikali kwa ufanisi uku wakizingatia uzalendo wa kuajili watanzania, itapelekea wizara yake kuendelee kuwaamini kwa kuwapatia miradi mingi .
“Serikali inawaamini ndiyo maana inawapa miradi mikubwa natamani hata mwende nje ya nchi maana itasaidia kuingiza pesa za kigeni kwenu hata kwa serikali tunaiona kazi yenu ni nzuri lakini jitaidini mkiwa mnaendelea na ujenzi mtenge barabara ya ziada ili kuwaondolea changamoto kubwa wananchi”
Kwa upande wao baadhi ya wananchi Maria Alfred, Plakiseda Frederick na Domisian Antony wakazi wa rubya wamemuomba mkandarasi anyejenga barabara ya kanyambogo rubya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda kwani imewaadhiri katika kufanya shughuli zao ususani katika harakati za kusafirisha wagonjwa kuwapeleka rubya ulazimika kuzunguka kupita barabara ya nshambya
Barabara ya Muhutwe kamachu yenye kilometa 5.5, Kanyambogo Rubya yenye kilometa10.2 na Muleba Kanyambogo kilometa 7.9 zinatekelezwa na serikali kwa kiwango cha rami.