Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwatiKamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwatiKamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha vipande viwili vya meno ya Tembo pamoja silaha haramu ambazo jeshi la polisi wamezikamata na nyingine zimerudishwa kwa hiyari na wananchi wa mkoa wa Iringa akiwa pamoja na Kamanda uhifadhi nyanda za juu kusin Joas makwati.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
JESHI la polisi mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha wamefanikiwa kukamata vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 34 katika kijiji cha
makongomi kata ya isalavanu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa tarehe 27.10.2022 majira ya saa 07:00 mchana huko katika kijiji cha makongomi kata ya isalavanu Wilaya ya Mufindi jeshi la Polisi Iringa kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha walifanikiwa kumkamata Crispin Muyinga miaka 35, mkulima wa makongomi akiwa na vipande viwili vya meno ya Tembo alivyokuwa amevificha kwenye msitu kwe mfuko wa salphet rangi nyeupe.
ACP Bukumbi alisema kuwa jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata Niko Kisinga mwenye umri wa miaka 40, mkazi wa Ilwazutwa na John Antony mwenye umri wa miaka 53, mkazi wa Mwanyenga wakiwa na nyamapori inayodhaniwa kuwa ya mnyama pofu iliyobanikwa na watuhumiwa hao walikutwa na vipande 60 vya nondo na baruti chupa mbili ambazo zote wanazitumia kwenye shughuli za uwindaji haramu.
Aidha ACP Bukumbi alisema kuwa jumla ya silaha kumi na tatu ambazo mbili ni aina ya Shortgun na kumi na moja ni aina ya Gobore ambazo zilisalimishwa katika vituo vya Polisi, ofisi za watendaji na maeneo mengine kwasababu mbalimbali zikiwemo wamiliki kuwa na umri mkubwa, na pia kutokuwa na uhalali wa umiliki baada ya kurithi silaha hizo kutoka kwa wazazi.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kutoa ushirikiano
kwa kuendelea kutoa taarifa mbalimbali za watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao baada ya muda wa kusalimisha kwa hiari kufika ukomo
ACP Bukumbi alimazia kwa kuyataja maeneo ambayo bado wamiliki wa silaha kinyume na sheria ambapo alisema “kutoka vyanzo vyetu vya taarifa bado kuna wananchi ambao wanamiliki silaha haramu maeneo yote ya hifadhi pamoja na mengine kama udekwa, Ruaha mbuyuni (Kilo lo), Wasa, Nyang’oro (Iringa) na Igoweko (Mufindi)”.