Mratibu wa Sera,Mipango na wa Utafiti wa Kituo cha Wanahabari,Watetezi na Taarifa (MECIRA) Gelard Hando akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara ya kituo hicho kuangalia vyanzo vya maji vya Mito ya Buthumi na Mgeta ambapo ni Chanzo kikubwa cha maji mto Ruvu.
Sehemu ya Mto Mgeta ukiwa na kina kidogo cha maji yanayokwenda mto Ruvu kwa ajili ya kulisha maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Mkazi wa Duthumi Shaban Mhina akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mto Duthumi unavyokauka kutokana na shughuli za kibinadamu
********************
*Wasema Mto Ruvu watakiwa jitihada za dharula kuunusuru
Na Mwandishi Wetu
Wadau wa Mazingira wameiomba Serikali kuchukua jitihada za kunusuru Mto Ruvu kutokana na vyanzo vyake vya maji mto huo kuingiliwa na shughuli za kibidamu zisizofuata utaratibu.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Sera ,Mipango na Utafiti wa Kituo cha Wanahabari,Watetezi Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Gelard Hando wakati taasisi hiyo ilipotembelea vyanzo vya majo katika mto Mgeta na Duthumi vilivyopo Mvuha mkoani Morogoro.
Hando amesema kuwa kina cha maji kilichofikia sio hali nzuri ya upatikanaji maji kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na hali hiyo imetokana na shughuli za kibidamu ya kuendesha kilimo na ukataji miti kwenye vyanzo vya maji.
Amesema kuwa kwenye suala hili hakuna mtu wa kulaumiwa ni jamii kujiuliza pale tulipokosea ambapo ni muda mwafaka wa kufanya kuweza kurudisha uoto kwa kuacha ukataji miti.
Hata hivyo wameshauro serikali kuangalia namna bora ya utunzaji maji kwa kuweka mabwawa ya muda yanayotokana na mito kuliko ilivyosasa maji yote yanapotelea karika bahari.
Amesema kuwa maeneo yaliyo katika vyanzo vya maji yamekuwa na ukame kwa kipindi kifupi ambacho kimechangiwa na ukataji mito na ufugaji usio zingatia uhifadhi wa maji.
Aidha amesema kuwa makundi ya mifugo katika mito yanasababisha kutokuwepo na chemu chem kutokana na kwato mifugo kushindilia.
Mkazi wa Bonye katika kijiji cha Buthumi Shaban Mhina amesema kuwa mto Duthumi kwa kipindi cha nyuma ulikuwa unafurika na kufanya shughuli zao uvuvi na kilmo cha umwagilia bila kuathiri mto lakini sasa hakuna hata samaki na hawawezi kutumia maji kwenye kilimo kutokana na kina hicho kupungua kwa ukataji miti na kuwa na mifugo mingi kwenye chanzo cha maji cha mto Ruvu.
Amesema kuwa serikali kazi kubwa kuangalia ufugaji wa makundi makubwa katika vyanzo vya maji yasiwepo ambapo ni muda mfupi kutarejea kuongezeka kwa kina cha maji.