Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Rashid Chuachua (wapili kulia) akifurahia baada ya kuzindua rasmi kampeni ya NMB Mastabta – Kotekote iliyozinduliwa kitaifa mkoani Mbeya yenye lengo la kuhamasisha malipo ya bidhaa na huduma kwa kutumia kadi, kuskani QR (Lipa Mkononi) na malipo ya kimtandao. Benki ya NMB Imetenga zawadi za zaidi ya milioni 300 kwaajili ya kampeni hii. Wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi, kulia ni Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Emmanuel Akonaay na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kadi, Philbert Casmir
…………………………
Msimu wa nne wa kampeni ya NMB MastaBata tayari umeanza baada ya promosheni hiyo ya kuchagiza malipo kidijitali kuzinduliwa Mbeya Ijumaa huku sehemu ya zawadi zenye thamani ya TZS milioni 350 ikipangwa kutumika kuwawezesha wateja kiuchumi.
Kiasi cha TZS milioni 173 na pikipiki 14 zitatumika kuwakwamua kiuchumi washindi wa shindano hilo linalojulikana mara hii kama NMB MastaBata, Kote-Kote!
Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw Filbert Mponzi, utaratibu huo utasaidia kuimarisha vipato vya wateja watakaoibuka washindi.
MastaBata ya mwaka huu itaua ndege wawili kwa jiwe moja. Itahamasisha matumizi zaidi ya kadi za NMB Mastercard na Lipa Mkononi(QR) na kuwapa fursa wateja kuboresha uchumi wao.
“Tofauti na mwaka jana, mwaka huu tumeamua kuwa na zawadi ya fedha pamoja na pikipiki sababu tunahitaji sio tu kuhamasisha matumizi ya kadi lakini pia kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi ya wateja wetu, tunaamini pikipiki hizi zinakwenda kutumika katika biashara na kuongeza kipato cha washindi wetu,” Bw Mponzi alibainisha.
Zawadi kubwa itakayohitimisha kampeni ya NMB MastaBata, Kote-Kote ni washindi saba kujishindia tiketi za kusafiri kuelekea Dubai pamoja na wenzi wao kwa siku nne
Kupitia zawadi hizo, NMB inataka na msimu unaokuja wa Krismasi na Mwaka Mpya kufana zaidi kwa wateja wake, na kusema kwani kila wiki wateja 75 watajishindia TZS 100,000 kila mmoja, Pikipiki moja na kila mwezi 1,000,000 kila mmoja na Pikipiki 2 hivyo jumla Pikipiki 14.
Mgeni rasmi wa uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dr Rashid Chuachua, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Bw Juma Homera na kuipongeza NMB kwa kuwa mshirika wa dhati wa maendeleo kuchangia ustawi wa jamii.
Huu ni mwaka wa wanne mfululizo wa kampeni za NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard kuhamasisha malipo bila kutumia pesa taslimu. Mchakato huu ulianza na MastaBata mwaka 2018, kisha MastaBata Siyo Kikawaida na kampeni ya mwaka jana ilikuwa ni MastaBata – KivyakoVyako.