Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza na wananchi wa Kata ya Irisya mkoani Singida mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kujitanbulisha ambapo pia alielezwa changamoto mbalimbali.
DC Mpogolo akisalimiana na viongozi wa Kata ya Irisya baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
DC Mpogolo akikagua mradi wa bomba la maji katika kata hiyo.
DC Mpogolo akikagua darasa katika Shule ya Msingi Kisuluda.
DC Mpogolo akizungumza na viongozi wa Kata ya Irisya wakati akikagua ujenzi wa vyumba vya maabara vya Shule ya Sekondari ya Irisya.
DC Mpogolo akizungumza na wanafunzi wa Sekobdari ya Irisya.
DC Mpogolo akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi Munyu.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Irisya, Haji Kingu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Afisa Tarafa ya Sepuka, Corlinel Nyoni akiwatambulisha viongozi kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Irisya, Ibrahim Kivando akizungumza.
Diwani wa Kata ya Irisya Ally Mwanga akizungumza.
Mkutano ukiendelea.
Mkazi wa kata hiyo Jumanne Mohammed akizungumza.
Simoni Muna akizungumza.
Samuel Mathayo akizungumza.
Mzee Iddi Ikuja akizungumza kuhusu migogoro ya ardhi.
Jumanne Mbihaji akizungumza.
Hassan Jumanne akizungumzoa kuhusu pembejeo. |
DC Mpogolo akiangalia moja ya darasa linalojengwa katika Shule ya Msingi ya Mwasutianga.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mwasutianga wakimuangalia DC Mpogolo (hayupo pichani) wakati alipokuwa shuleni hapo.
DC Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Irisya baada ya kumaliza ziara yake.
Na Dotto Mwaibale, Singida
VIJIJI 74 wilayani Ikungi mkoani Singida vinatarajia kupata umeme wa Wakala wa Umeme vijijini (REA) ifikapo mwaka 2020.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Irisya katika mkutano wa hadhara alipofanya ziara ya
kukagua miradi na kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dkt7.Johh Magufuli kuwa DC wa wilaya hiyo.
” Vijiji 74 katika wilaya yetu vitapata umeme wa REA awamu ya tatu hivyo jiandaeni kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwani hiyo ni fursa kwenu” alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema katika wilaya hiyo kuna vijiji 101 na kata 28 na makao makuu zilipo kata hizo karibu zote tayari zimepata umeme kasoro chache na dhamira ya Rais Dkt. John Magufuli nikuona ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote na vitongoji vinakuwa na umeme.
Wakizungumza katika mkutano huo wananchi hao walieleza changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni kuwa na daktari mmoja katika Kituo cha afya katika kata hiyo hali inayoleta usumbufu pale anapopata dharura.
” Tunakuomba DC wetu utusaidie tupate daktari na muuguzi katika zahanati yetu ambayo inauhaba wa watumishi baada ya waliokuwepo kuhamishwa na kubaki mmoja” alisema Jumanne Mohammed.
Samuel Mathayo alisema kutokana na zahanati hiyo kutoa huduma kwa vitongoji vingine vilivyo jirani na Irisya aliomba ipandishwe hadhi na kuwa kituo cha afya ili kukabiliana na wingi wa wagonjwa.
Kwa upande wake Simoni Muna aliomba ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Munyu ukamilike haraka ili kuwapunguzia adha ya kutembea zaidi ya kilometa tatu watoto wanao ishi katika eneo hilo kwenda kusoma Shule ya Msingi ya Irisya.
Mkazi mwingine wa kata hiyo Iddi Ikuja aliiomba serikali kusaidia kutatua migogoro ya ardhi ambayo ni mingi inayosababishwa na watu kuvamia mashamba ya wenzao wakidai ni yao.
Juma Mbihaji alitaka kujua serikali inampango gani wa kutoa ajira kwa watoto wao ambao wamemaliza masomo lakini wapo kijijini hapo mwa muda mrefu bila ya kuwa na kazi.
Diwani wa kata hiyo Ally Mwanga aliomba mradi wa maji uliopo katika kata hiyo uharakishwe ili uanze kufanya kazi kwa kununua mabomba na vifaa vya usambazaji.
“Tayari serikali ilikuja kupima maji na kufanya majaribio ambapo maji yalitoka kwa wingi na kuleta furaha kwa wananchi kwani tangu kata hii ianzishwe hatujawahi kuwa na bomba la maji zaidi ya kutumia ya visimani” alisema Mwanga.
Alisema maji yaliyopatikana yanauwezo wa kutoa lita 18,000 kwa saa ambapo ni sawa na pipa 740 na kuwa kata hiyo itajitosheleza na ziada itakwenda katika vitongoji vingine vya jirani vya Munyu na Masutianga.