Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa maagizo kwa idara ya mipango mijikumaliza mgogoro wa ardhi katika mlima Igereke
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa maagizo kwa idara ya mipango mijikumaliza mgogoro wa ardhi katika mlima Igereke
Fausta Timoth Kitindi ni bibi anayekadiliwa kuwa na zaidi ya miaka miaka 70 akitoa malalamiko yake kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuhusu madai yake ya kudhurumiwa ardhi
Na
Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa mwezi mmoja idara ya mipango
miji kuhakikisha wanatatua mgogoro ya mipaka katika eneo la mlima Igeleke
uliopo kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa baina ya wananchi na kikundi cha uhifadhi
wa mazingira KIUMAKI.
Akizungumza
kwenye Mkutano wa hadhara,mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa idara ya mipango
miji inatakiwa kufanya kazi haraka ya kuitambua mipaka ya mlima Igeleke na
maeneo ya wananchi.
Moyo
alisema kuwa amegundua kuwa kuna mapungufu waliyoyabaini katika nakala ya
mkataba uliowapa mamlaka KIUMAKI kujihusisha na uhifadhi katika eneo hilo hivyo
ni muhimu ukapitiwa ili kujiridhisha.
Alisema
kuwa kufuatia mapungufu ya kimkataba ikiwemo kuwepo kwa Mashaka ya uhalali wa
mkataba huo baina ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na KIUMAKI
na kuamuru mkataba huo kuwasilishwa katika ofisi mapema kesho asubuhi Ili uweze
kupitia na kamati ya Ulinzi
Lakini
pia mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliamuru kukamatwa Kwa Mtu
yeyote atakayebainika kufanya shughuli za kibinaadam katika hifadhi ya Igeleke
wakati huu serikali ikishughulikia Mgogoro baina ya Wananchi na kikundi Cha
uhifadhi Cha KIUMAKI.
Moyo
alimazia kwa kuwaomba wananchi wa mtaa wa Kihesa Kilolo A na B kuwa na
subira wakati serikali ya wilaya ikiwa inautafutia ufumbuzi mgogoro huo.
Kwa
upande wa wananchi wa Kihesa Kilolo A na B walisema kuwa kikundi cha KIUMAKI
kimepora ardhi ya eneo hilo kwa kutumia mabavu kwa madai kuwa kikundi hicho
kinachojihusisha na utunzaji wa Mazingira katika Mlima Igeleke yalipo
makumbusho ya michoro ya kale.
Fausta
Timoth Kitindi ni bibi anayekadiliwa kuwa na zaidi ya miaka miaka 70 alisema
kuwa Amekuwa akikumbana na bughudha ya Mgogoro huu huku eneo
aliloachiwa na wazazi wake pamoja sehemu kaburi kutajwa na kikundi hicho kuwa
ni eneo lililo chini ya Hifadhi.
Awali
Katibu wa KIUMAKI Filipo
Mkwama alisema walichukuwa maeneo hayo na kuanza kuyaifadhi kwa kufuata
taratibu na sheria za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kuingia mkataba
baina ya kikundi hicho na uongo wa Manispaa ya Iringa.
Hata
hivyo Kaimu Afisa Ardhi wa Manispaa ya Iringa Priscus Shirima ameshauri
baadhi ya masuala muhimu kufanyika huku akitoa hakikisho la kuanishwa Kwa
mipaka ya eneo hilo.