*************************
Na Mwandishi wetu, Babati
“MANGOCHI Junior Sekondari kauli mbiu ya shule yetu ni jifunze leo ili uongoze kesho,” hivyo ndivyo Mkurugenzi wa shule ya sekondari Mangochi Junior iliyopo Malangi Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Ernest Sanka anavyoanza kuzungumzia juu ya shule hiyo.
Sanka anasema shule ya sekondari Mangochi Junior ni mpya na wanafundisha wanafunzi wao kwenye masomo na maadili mema kwenye taaluma ili wawe watu wema kwa miaka ijayo.
Anasema shule hiyo inapokea wanafunzi wa dini zote na kuwalea vizuri kiakili, kimwili na kiroho, imesajiliwa kwa mitihani ya kidato cha nne kwa reg.no.S5620 hivyo wanaotaka kurudia mitihani ya kidato cha nne (QT na PC) wanawakaribisha wote.
Anasema shule yao ipo mtaa wa Malangi, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara na ina mazingira mazuri na walimu wa kutosha wa kutoa elimu bora.
“Shule hii ni ya bweni kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na ya mchanganyiko yaani wavulana na wasichana, ambapo masomo tisa yanafundishwa shuleni hapa pamoja na English course na pre-form one,” amesema Sanka.
Anasema ada yao ni nafuu kwani kwa mwaka ni shilingi milioni 1.2 na wazazi na walezi wanaruhusiwa kulipa ada yao kwa awamu moja, mbili au tatu kwa mwaka.
Amesema wameanza kufundisha masomo ya pre-form one kuanzia Oktoba 10 hadi Desemba 8 mwaka 2022 na ada ya pre-form one kwa wanafunzi wa kutwa ni shilingi 25,000 kwa mwezi na wanafunzi wa bweni ni shilingi 50,000 kwa mwezi na masomo hayo yanafanyika kwa muda wa miezi miwili.
“Mzazi au mlezi mlete mtoto wako shuleni Mangochi Junior kwa elimu bora, karibu kwa mawasiliano unaweza kupiga kwa Mkurugenzi wa shule kwa namba 0755 777 114 Mkuu wa shule kwa namba 0627 562 529 au 0786 818 872 namba ya mapokezi shuleni ni 0624 222 555,” amesema Sanka.
Mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Mussa Salimu anawakaribisha wazazi na walezi wenye watoto wanaohitaji kuanza kidato cha kwanza kuwafikisha shuleni hapo watoto watoto wao.
Mwalimu Salimu amesema shule yao inafundisha taaluma bora kwa wanafunzi wote na wanafunzi wa kutwa watahudumiwa chai ya asubuhi na chakula cha mchana tu na wale wa bweni watahudumiwa milo minne kwa siku.
“Ukisoma pre-form one kwetu hautafanya mitihani ya usaili kuingia kidato cha kwanza na kwa kidato cha kwanza usaili awamu ya kwanza itaanza Novemba 15 saa 2 asubuhi na awamu ya pili itaanza Novemba 26 saa 2 asubuhi,” amesema mwalimu Salimu.
Amesema wanafunzi watakaokaa bweni kipindi cha pre-form one watapunguziwa ada ya shilingi 100,000 kwenye ada ya kidato cha kwanza kwenye mwaka 2023.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule hiyo, Patricia Alex anasema mazingira ya shule hiyo ni mazuri kwa wanafunzi kwenye kusoma, taaluma ni bora, chakula na malazi ni mazuri.
“Tunasoma vizuri mchana na jioni inapofika tukishakula chakula tunasali na kujifunza masomo ya dini kwa wanafunzi wa madhehebu tofauti, hivyo tunawashukuru wazazi, walimu na uongozi wa shule,” anasema Patricia.
Mwanafunzi mwingine wa kidato cha kwanza wa shule hiyo Daniel Godfrey ambaye ametokea mtaa wa Ngaramtoni Mkoani Arusha, anasema amevutiwa kusoma kwenye shule hiyo kutokana na taaluma inayotolewa.
“Wazazi na walezi wenye watoto wanaohitaji kusoma shule ya sekondari, wawalete hapa Mangochi Junior kwa ajili ya kujiunga nasi na kupata elimu bora,” anasema Godfrey.
Mwanafunzi wa Pre-form one Isdore Francis anasema amezungumza na wazazi wake na kuwasihi wafuate taratibu za yeye kujiunga na shule hiyo kusoma kidato cha kwanza kwani ni shule nzuri inayotoa taaluma bora na mazingira mazuri.