**********
Na Anjela seth
Imebainishwa kuwa idadi ya vifo vitokananvyo na matumizi ya kemikali zenye madhara kiafya na kimazingira inazidi
kuongezeka hivyo inahitajika elimu ya kutosha kuepukana na madhara yatokanayo na kemikali hizo.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ambayo yameandaliwa na shirika la umoja wa kimataifa linalohusika na utafiti kwa kushirikiana na ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ya Tanzania.
Amesema kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na matumizi ya kemikali hatarishi hadi kufika mwaka 2019 ilifikia watu milion mbili nakwamba inaweza kuongezeka maradufu endapo elimu haitaendelea kutolewa.
Dkt Mafumiko amesema kuwa mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu wa serikali pamoja na sekta binafsi kuweza kujadili kwa pamoja nakuwa na uelewa mpana wa namna yakuepukana na matumizi ya kemikali hatarishi kwa binadamu na mazingira.
“Ofisi yangu imeshirikiana na shirika la umoja wa kimataifa linalohusiana na tafiti kufanya mafunzo haya ya mfumo wa kidunia wa kufuatilia usafirishaji wa kemikali kutoka zinapozalishwa hadi kwa watumiaji pamoja na kuwa na alama za utambuzi wa kemikali hizo ili kuwezesha kuepikana na madhara yatokanayo na kemikali hizo ikiwemo vifao” amesema Dkt Fidelice Mafumiko
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo afisa Sera Mazingira ya Biashara kutoka shirikisho la Viwanda Nchini CTI Anna Kimaro amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuchukua tahadhari ya matumizi ya kemikali hatarishi kwenye maneo yao ya kazi.
“Wanachama wetu ndio watumiaji wakubwa wa kemikali, mafunzo haya yatatusaidia kuondoa madhara ya kemikali kwenye viwanda nakuweka alama za utambuzi wa kemikali hizo” ameaema Anna.