Mkurugenzi
wa VETA Kanda ya Kati Dodoma, John Mwanja akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa chuo
hicho kwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye (kushoto), wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua ujenzi wa chuocha VETA wilayani Ikungi mkoani hapa juzi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini
(TAKUKURU) Neema Mwakalyelye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ikungi. Kutoka kulia waliosimama mbele ni ni
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Ikungi, Erick Nyoni, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa
Singida,Widege Mzalendo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Jerry Muro, Mwenyekiti wa CCM
wa wilaya hiyo, Mika Likapakapa na Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Dodoma,
John Mwanja. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Ikungi (OCD) Suzana Kidiku na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo,
Winfrida Funto.
Na
Dotto Mwaibale, Singida
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi (VETA) imetoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini na kutoa fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyuo vipya na uboreshaji wa vyuo vya zamani.
Pongezi hizo zimetolewa
juzi na Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Dodoma, John Mwanja mbele ya Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU)
Neema Mwakalyelye kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa VETA wakati wa kikao na
viongozi mbalimbali wa wilaya ya Ikungi cha kupata taarifa ya ujenzi wa chuo
cha ufundi VETA kilichojengwa wilayani humo na VETA Kanda ya Kati-Dodoma kwa usimamizi
wa TAKUKURU.
Aidha
Mwanja alitoa shukurani hizo za dhati kwa Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU Neema Mwakalyelye kwa usimamizi thabiti katika shughuli za serikali hivyo kuifanya serikali ya Awamu ya sita ing’are katika kuwaletea wananchi maendeleo yao.
Katika
hatua nyingine Mwanja alitoa shukrani kwa uongozi wa chama na serikali wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Ikungi kwa ushirikiano wao mkubwa wanaowapa katika kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ikungi.
Akizungumzia
faida ya chuo hicho mara kitakapokamilika alisema kinatarajiwa kuhudumia wakazi
wapatao 343,985 wa Wilaya ya Ikungi na wakazi
wapatao 1,754,370 wa
Mkoa wa Singida.
Pia, wakazi wa
mikoa jirani watanufaika
na huduma za chuo.
.
Alisema
katika utaoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwenye kozi za muda mrefu na
kozi za muda mfupi, chuo hicho kitajielekeza katika
kutoa mafunzo kwenye
maeneo ya kimkakati
kulingana na mahitaji ya shughuli
za kiuchumi wanazofanya wananchi wa Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kwa
ujumla.
Alisema
katika kutekeleza mradi huo VETA imekumbana na changamoto mbali mbali kama
kupanda kwa
bei ya vifaa
vya ujenzi wakati
wakiendelea na utekelezaji
wa mradi, hali iliyopelekea pesa
iliyotengwa kutokidhi mahitaji
halisi ya mradi
kutokana na bei
za vifaa kupanda zaidi ya
matarajio ya awali.
.
Alitaja changamoto nyingine
waliyokumbana nayo ni uwezo mdogo wa kiuchumi wa mafundi waliowatumia hivyo
kupelekea kushindwa kuwalipa vibarua wao kwa wakati na kupelekea baadhi yao
kuacha kazi, hivyo kupelekea kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi.
“Sisi watumishi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) husunani VETA Kanda
ya Kati tunaahidi kuendelea kutekeleza mradi huu na mingine yote kwa uadilifu
mkubwa, na kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo
mbalimbali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Mwanja.