Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bukoba-BUWASA jana tarehe 19/10/2022 amekabidhi mradi wa maji uliopo Bisheshe Wilayani Karagwe kwa BUZUBONA &SONS COMPANY Limited ili kukamilisha kazi zilizobaki ambapo hapo awali ulikuwa ukitekelezwa na Wataalamu wa ndani.
Kazi ambazo amekabidhiwa Mkandarasi huyo ni pamoja na Ujenzi wa vilula 12, Ulazaji wa bomba km 16,Ujenzi wa line ya umeme km 2 pamoja na ujenzi wa chanzo.
Muda wa utekelezaji wa mradi huo ni miezi 6 na gharama ya utekelezaji wa mradi huu ni Tshs 532,911,491.95 na unatarajiwa kuhudumia wakazi 8016.
Akiongea baada ya makabidhiano hayo Mkandarasi aliwahakikishia viongozi mbalimbali wa kata hiyo kukamilisha mradi huu ndani ya muda uliopangwa kuisha.