***********
NA.Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO amewataka madereva na wamiliki wa matrekta katika Mkoa wa Arusha kufuata sheria za usalama Barabarani Ili kupunguza ajali ama kumazimaliza ajali katika Mkoa huo.
SP Solomon Mwangamilo amesema hayo leo October 20 alipokuwa akizungumza na Madereva na wamiliki wa Matrekta katika kata ya Kikatiti wilaya ya Arumeru Mkoa Arusha ambapo amebainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinasabibishwa na vyombo hivyo kwa kukosa viakisi mwanga(reflectors).
Ametoa muda wa mwezi mmoja kufanya ukarabati wa vyombo hivyo nakuweka viakisi mwanga (reflectors) ili kupunguza ajali ambazo zina gharimu Maisha ya watu
Nao baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo hivyo wamesema semina na maelekezo waliyoyapata wameshapokea ambapo wamebainisha kuwa hapo mwanzo walikuwa hawana uelewa juu ya madhara ya kutoweka viaksi mwanga.