Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotoa zawadi ya sh. milioni moja kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe, Leocadia Vedastus (kulia), Diwani wa Kata ya Irugwa Joseph Sabato (wa pili kulia) na Mtendaji wa Kata hiyo Ada Sijo (wa pili kulia) katika mkutano aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe Oktoba 17, 2022.Alitoa zawadi hiyo baada ya kuvutiwa na usimamizi mzuri wa sh. milioni 250 zilizotolewa na Seriali Kuu kujenga madarasa sita shuleni hapo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama madawati wakati alipokagua madarasa sita katika Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe ambayo yamejengwa kwa sh. milioni 120 zilizotolewa na serikali kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Oktoba 17, 2022. Pia zilitumika kununua madawati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua madarasa sita katika Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe yaliyojengwa kwa sh. milioni 120 zilizotolewa na serikali kuu, ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Oktoba 17, 2022. Pia zilitumika kununua madawati. Kushoto kwake ni Mkuu wa Shule hiyo, Leocadia Vedastus. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Irugwa wilayani Ukerewe ,Leokadia Vedastus wakati alipokagua madarasa sita yaliyojengwa kwa sh. milioni 120 zilizotolewa na serikali kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Oktoba 17, 2022. Pia zilitumika kununua madawati. Kulia ni Diwani wa Kata ya Irugwa, Joseph Sabato wote wawili walishirIkiana kusimamia ujenzi huo ambao ulimvutia sana Mheshimiwa Waziri Mkuu hadi akawazawadia sh. Milioni moja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kizungumza na watoto Katondo Kebele (kushoto), Wilhelemina Mafele (katikati ) na Gozibert Bwere ambao walishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha Utandawazi cha Ukerewe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe Oktoba 17, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua madarasa sita katika Shule ya Sekondari Iirugwa wilayani Ukerewe yaliyojengwa kwa sh. milioni 120 zilizotolewa na Serikali Kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola, Oktoba 17, 2022. Pia zilitumika kununua madawati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa madarasa sita katika Shule ya Sekondari Irugwa wilayani Ukerewe ambayo yamejengwa kwa sh. milioni 120 zilizotolewa na serikali kuu ambazo zilibaki na zikatumika kujenga matundu ya vyoo, mabafu na mfumo wa kuvuna maji ya mvua na umeme wa sola. Pia zilitumika kununua madawati. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua madararsa hayo Oktoba 17, 2022 na kufurahishwa na matumizi mazuri ya fedha hizo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)