NA FARIDA SAIDY ,MOROGORO
MKUU wa wilaya ya Malinyi Bw. Mathayo Masele amesema anafahamu changamoto mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo ikiwemo Afya na Elimu hivyo atajitahidi kushirikiana na watendaji wa serikali na wananchi ili kuzitatua changamoto hizo
Mkuu wa wilaya huyo ameyasema hayo mara baada ya kula kiapo cha utumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro ambapo amesema Rais Magufuli amemuami ndomana amemteua hivyo atahakikisha anajitahidi kutauatua changamoto zinzowakabili wananachi wa wilaya hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemtaka mkuu huyo wa wilaya kusimamia kikamiligu fedha za miradi ya serikali inayotekelezwa na seruikali wilayani hapo huku katibu tawala mkoa Huo mhandisi Emanuel Kalobero amesema lengo la Rais Magufuli ni kuwaletea manedeleo wananachi hivyo viongozi ambao wameaminiwa wanatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya uongozi
Aidha Bi. Regina Chonjo ni mkuu wa wilaya ya Morogoro amemshauri mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Malinyi kuangalia dira ya viongozi wakubwa wa kitaifa katika utendaji wa kazi.