Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa anaetarajia kufanya ziara Mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (kulia) akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya ujio wa Waziri Mkuu.
***********************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo ata kagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 13,2022 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima, amesema Waziri Mkuu atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Daraja la Magufuli,mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi na kuzindua jengo la huduma ya macho kwenye Hospital ya Kanda ya Rufaa Bugando.
“Oktoba 17,2022 Waziri Mkuu atatembelea Wilaya ya Ukerewe ambapo atawasili kwenye kisiwa cha Irugwa kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya,ujenzi wa shule ya sekondari Irugwa”, ameeleza Malima
Katika hatua nyingine Malima ametoa rai kwa madereva na wamiliki wa magari kuwa na utaratibu wa kuondoa magari pindi yanapoharibika barabarani ili kuepusha msongamano unaoweza kusababisha ajali zisizokuwa za lazima.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi, ameeleza mikakati mbali mbali iliyopo ya kuhakisha wanapunguza ajali za barabarani ikiwemo askari kusimamia maeneo ya watembea kwa miguu.