Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga. |
Naibu
Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa siku ya
kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi
Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa siku hiyo
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Isihaka
Mirambo akizungumza wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani
iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.
MRATIBU wa Watoto Jiji la Tanga Mwajuma Mustapha akizungumza wakati wa maadhimisho hayio
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
MWAKILISHI
wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo amesema kwamba
wao wamejikita katika harakati za kuwasaidia watoto wa kike kukabiliana
na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa utekelezaji wa mradi wa
elimu kwa mkoa wa Tanga ili kuwawezesha waliokosa fursa hiyo kunufaika
nayo.
Katika mradi huo wa elimu Shirika hilo limekuwa likitoa
fursa za elimu ya awali yaani ECD kwa watoto wadogo ikiwemo watoto wa
kike na elimu ya Sekondari kwa mabinti walio nje ya mfumo rasmi wa elimu
kwa kutumia programu ilioharakishwa Accelerated Learning Program (QT).
Hayo
yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac
Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa
kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.
Isihaka
ambaye ni Msimamizi wa Miradi ya Elimu wa Shirika la Brac Maendeleo
Tanzania Mkoani Tanga alisema kwamba katika utekelezaji wa mradi huo
wameweza kuwafikia mabinti wengi ambao wamenufaika kupitia miradi yao.
Alisema
kwa upande wa wanufaika wa shule za Sekondari mabinti 926 ambao wengine
wapo katika ngazi tofauti tofauti kama vile wasichana 10 wapo vyuo
vikuu mbalimbali nchini, wasichana 51 wapo kidato cha sita ,wasichana 25
wamehitimu katika vyuo vya kati mbalimbali nchini na wengine wapo
katika ngazi ya Sekondari katika shule huria mbalimbali hapa Tanga.
Alisema
pia wanufaika takribani 1376 wamepatiwa mafunzo mbalimbali yahusuyo
elimu ya Afya ya Uzazi, Athari zitokanazo na matumizi ya dawa za
kulevya, Ujasiriamali nk ikiwemo kuwawezesha vifaa kwa ajili ya kuanza
shughuli za uzalishaji katika Jamii kwa lengo la kujiongezea kipato
katika nyanja walizosomea kama vile ushonaji, utengenezaji wa batiki,
sabuni na mapishi.
“Lakini pia watoto takribani 2100 tumewapatia
elimu ya awali katika vituo vyetu vya malezi na makuzi vilivyopo katika
shule za Serikali za Msingi Mkoani Tanga huku watoto wengine 772
wanaendelea kunufaika na elimu hiyo nchini ya Ufadhili wa NORAD na Brac
Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa mradi huu “Alisema.
Awali
akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana alitoa wito kwa watoto wa
kike wasikubali kurubuniwa.
Dkt Sipora alisema kwamba Rais Samia
Suluhu amewajali sana watoto wa kike ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi
wa madarasa bilioni 580 kwa ajili ya madarasa 29 na mwaka jana alitoa
Bilioni 1.8 zaidi ya hapo alitoa Bilioni 2 ya madarasa.
Alisema
pia Rais Samia alitoa fedha nyengine zaidi ya Bilioni 700 kwa ajili ya
watoto wa kike timiza malengo kila mtoto 250,000 kwa ajili ya kuanzisha
miradi ili kuepukana na vishawishike watoto wa kike waliopo mitaani .
“Lakini
pia bado kwenye mapato ya ndani Rais Samia ametoa asilimia 10 ya mapato
inaenda kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu huko ndani wengi ni
wanawake watoto wa kike”Alisema.
Awali akizungumza wakati wa
maadhimisho hayo Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo bado watoto
wa kike wana jukumu la kufanya ili kuondokana na adha ya kukosa
maendeleo.
” Kama mlivyomsikia MC hapa amesema kwamba wapo
watoto wenyewe wanawashawishi wajomba acheni tabia na tambueni jukumu
lenu la kuleta maendeleo endelevu” Alisema
Naibu Meya huyo
alitoa wito kwa watoto wa kike kuhakikisha wanasoma kwa bidii maana
elimu pekee ndio inaweza kuwakomboa na watambue kwamba hakuna bahati
ila waamini kwamba elimu ndio itawawezesha kuwakwamua .
Hata
hivyo aliwatoa hofu watoto wa kike kwamba Serikali imeendelea kuuunga
mkono juhudi za watoto wa kike kuhakikisha wananufaika na uwepo wa fursa
mbalimbali zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.