Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada yaliyofanyika leo Oktoba 11,2022 Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada yaliyofanyika leo Oktoba 11,2022 Jijini Dar es salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada yaliyofanyika leo Oktoba 11,2022 Jijini Dar es salaam. Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada yaliyofanyika leo Oktoba 11,2022 Jijini Dar es salaam.
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kwa mara ya kwanza, jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wadau wa elimu nchini, wameshuhudia wanufaika wa kwanza wa ufadhili wa wanafunzi wenye ufaulu wa juu katika mtihani wa kidato cha sita katika masomo ya sayansi, UDSM Merit Scholarship, wakiwa miongoni mwa wahitimu wa mahafali ya 52.
Ameyasema hayo leo Oktoba 11,2022 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Amesema kwa wale wa programu za miaka mitatu, idadi ya wahitimu ni kumi na tano, kati ya hao wanafunzi tisa wamepata daraja la kwanza. Kati ya hao tisa, wasichana ni watano ambao ni asilimia 55%.
Aidha amesema mwanafunzi mwenye ufaulu wa juu anawakia wa 4.8 kati ya 5. Kwa upande mwingine, wanafunzi sita wamepata daraja la pili wakiwa na wakia wa chini ya 4 na 5.
Pamoja na hayo amesema ili kukabiliana na changamoto ya usafiri wa wafanyakazi, chuo kilinunua mabasi mawili kwaajili ya usafiri wa wafanyakazi.
“Basi moja limeanza kuwahudumia wafanyakazi katika Kampasi ya Mwalimu Nyerere Mlimani na basi la pili linatumika kwenye Taasisi yetu ya Sayansi za bahari iliyoko Zanzibar”. Amesema Prof.Anangisye.
Amesema ili kukabiliana na changamoto za ajira kwa wahitimu wa taasisi mbalimbali za elimu, Chuo kilianzisha mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wote bila kujali vyuo walivyosomea.
“Kila mwaka mafunzo haya hufanyika katika mikoa 10 ya Tanzania bara na visiwani. Kwa mwaka huu mafunzo yatafanyika Dar es Salaam, Dodoma, Unguja, Pemba, Tabora, MwanzaMbeya na Ruvuma”. Amesema
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mafaniko makubwa katika kuwajengea wahitimu wa vyuo mbalimbali uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine.