Meneja wa mawasiliano Dawasa wa kushoto Everlasting Lyaro akitoa maelekezo kwa Naibu wa uwekezaji na biashara Exavd Kigahe alipotembelea katika Banda la Dawasa.
……………………
Na Victor Masangu,Pwani
Naibu Waziri waziri wa Wizara ya uwekezaji na biashara Exavd Kigahe ameitaka Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mangira (DAWASA) kuweka mipango ya kukabiliana na winbi la upotevu wa maji unaofanywa na baadhi ya wananchi kuharibu miundombinu ya mabomba.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kilele cha wiki ya maonesho ya tatu ya uwekezaji na biashara Mkoa wa Pwani na kusema kwamba kunahitajika juhudi za makusudi ya kudhibiti hali hiyo kwani serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maji.
Aidha Naibu Waziri huyo alitoa pongezi kwa juhudi mbali mbali zinazofanywa na Dawasa katika kuwahudumia wananchi huduma ya maji safi na salama na kuwataka kuendelea kuvilinda zaidi vyanzo vya maji lengo ikiwa ni kuwa na uhakika wa maji katika kipindi chote.
“Kitu kikubwa ambacho kinatakiwa ni kuweka mikakati endelevu ambayo itaweza kusaidia katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji s ambamba na miundombinu yake ya mabomba ili maji yasiweze kupotea bure katika maeneo iliyopo miradi.
Katika hatua nyingine aliiomba Dawasa kuendelea kutekeleza miradi yake ipasavyo katika maeneo ya Mkoa Dar es Salaam pamoja na Pwani ikiwemo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji.
Kwa Upande wake Meneja mawasiliano wa Dawasa Everlasting Lyaro alibainisha kwamba kwa sasa kiwango cha upotevu wa maji kimefikia asilimia 38 na kwamba wanaendelea kuweka jitihada zaidi katika kupambana na hali hiyo ya upotevu wa maji kwa wakazi wa Pwani na Dar es Salaam.
Kadhalika Meneja huyo aliongeza kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wanakabiliana na changamoto hiyo ya upotevu wa maji na kuongeza kuwa utekelezaji wa miradi mbali bado unaendelea vizuri kwa lengo la kuwahudumia wananchi waweze kupata maji Safi na salama.
Pia alitoa wito kwa wananchi kuachana na tabia ya kuharibu miundombinu ya maji kwani kufanya hivyo ndio kunapelekea kuwepo kwa baadhi ya maeneo kuwa na upotevu wa maji na kuahidi kulifanyia kazi kwa maslahi ya wanachi wote.
Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (Dawasa) imeweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya tatu ya wiki ya uwekezaji na biashara na kuweza kutoa elimu na ushauri kwa baadhi ya wananchi walioweza kutembelea katika banda lao.