Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Joseph Buchweishaija akiongea na Menejimenti ya Chuo wakati wa kuwakaribisha Manaibu Wakuu wa Chuo hicho, Oktoba 10,2022 Kampasi ya Tengeru Arusha.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Joseph Buchweishaija (kushoto) akimtambulisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino (kulia) wakati wa kikao na Menejimenti ya Chuo Oktoba 10,2022, katikati aliyekaa ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Joseph Buchweishaija (kushoto) akimtambulisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (Katikatialiyesimama) wakati wa kikao na Menejimenti ya Chuo Oktoba 10,2022, Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino .
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Joseph Buchweishaija (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Emmanuel Luoga (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino ( wa pili kulia) ,na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (wa kwanza Kushoto) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala anayemaliza muda wake Profesa Charles Lugomela ( wa kwanza Kulia) pamoja na Menejimenti ya Chuo Oktoba 10,2022.
………………………………….
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Prof.Joseph Buchweishaija amewataka watumishi wa Chuo hicho kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya ambao ni Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa. Suzana Agustino na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa. Antony Mshandete walioteuliwa Septemba, 2022 na Mkuu wa Chuo hicho Dr. Mohammed Gharib Bilal.
Professa Buchweishaija ameyasema hayo Jijini Arusha katika Kampasi ya Chuo hicho wakati wa kuwakaribisha viongozi hao kwa Menejimenti, Watumishi na Wanafunzi wa chuo hicho.
Aidha, Buchweishaija amesisitiza kuwa ili kuleta maendeleo ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa weledi, kujitoa na kujituma ili kufikia malengo yaliyowekwa na kuleta maendeleo kwa Taasisi na jamii kwa ujumla.
“Ushirikiano,kujituma na kufanya kazi kwa weledi ndiko kunakoleta mafanikio hivyo ninawaomba mzingatie hayo “amesema Profesa Buchweishaija.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Emmnauel Luoga amewapongeza viongozi hao wapya na kumshukuru Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala aliyemaliza muda wake Profesa Charles Lugomela kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chote cha miaka minne.
Vilevile, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino ameahidi kuitumikia Taasisi hiyo kwa uaminifu, weledi, juhudi na maarifa katika kuhakikisha taasisi hiyo inazidi kusonga mbele.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ubunifu mpya Profesa Antony Mshandete ameahidi kushirikiana na viongozi ,Watumishi na wanafunzi katika kutekeleza majukumu ya kila siku ili kuijenga Taasisi ya Nelson mandela.
Halfa hiyo ya kuwakaribisha viongozi hao wapya walioteuliwa Septemba 2022 , iliambatana na ziara ya kutembelea maeneo ya mbalimbali ya Chuo ikiwemo Maabara, Maktaba, Vituo vya Umahiri pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi unaotekelezwa na Taasisi hiyo.