*******************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba,Kagera
Ni katika kongamano la vijana amalo kitaifa linafanyika mkoani kagera kongamano ambalo limewashirikisha vijana kutoka katika sehemu mbalimbali kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar ikiwa kilele cha maadhimisho hayo ni October 14 mwaka huu ambapo mkuuwa mkoa wa kagera amewataka vijana kutumia fursa zinazojitokeza na kuacha kulalamikia serikali kuwa aitoa ajira.
Akizungumza katika kongamano hilo mkuu huyo wa mkoa mh. Arbert .J. Chalamila lililofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba kwa niaba ya mgeni rasmi waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,Ajira,Vijana na wenye ulewmavu mh. Joyce Ndalichako amesema kuwa vijana walio wengi wamekuwa awajitokezi katika kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika jamii na hata katika halmashauri zao.
“vijana muache kulalamika lakini pia licha ya vijana kutojishughurisha wapo watu wazima ambao wanawafanya vijana kutotumia fursa hizo kwakuwa na tabia ambazo aziwashawishi vijana badara yake tunazalisha taifa lenye vijana wavivu na walalamikaji”
Pia mkuu huyo wa mkoa amewataka vijana waliofanikiwa katika ngazi tofauti kuwapa hamasa vijana ambao bado awajafikia malengo yao ili kuweza kuwafanya kujikwamua katika maeneo mbalimbali kwa kuchangamkia fulsa na kuzifanyia kazi fursa hizo zinazojitokeza.
Aidha nae mkurugenzi idara ya maendeleo ya vijana Tanzania bara ndg. Mwija Mbeki amesema kuwa mpaka sasa serikali imejipanga kumuwezesha kijana mmoja mmoja kuhakikisha anafikia malengo yake kwa kutoa mkopo mpaka shilingi milioni 50 kuliko kupitia katika vikundi kama ilivyozoeleka.
“serikali tumejipanga kwa kushirikiana na ofisi ya waziri mkuu kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu kuhakikisha kila kijana anajikwamua kiuchumi ambapo tumetengeneza sera na kanuni itakayo mfanya kijana mmoja mmoja kujitegemea ikwa serikali itaridhika na ufanyaji kazi na ujishughurishaji wake kwani pesa hizi tunategemea kufikia Desember mwaka huu zitakuwa zimefika katika halmashauri ili kuondo changamoto ya vijana kujiunga kwenye vikindi”.amesema mbeki