Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Baraza la Maulid la kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad(S.AW) ambalo Kitaifa limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana mara baada ya kumalizika kwa Baraza la Kitaifa la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 09 Oktoba 2022.
Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria na kuhutubia kwenye Baraza la Maulid ambalo Kitaifa limefanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha (kushoto) ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla
Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa kwenye Baraza la Maulid kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad(S.AW) ambalo Kitaifa limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Oktoba, 2022.