Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (kulia) akikata utepe wakati wa hafla ya mgodi wa Barrick Bulyanhulu kukabidhi Mashine 2 za Biohazard safety cabinet katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga na kituo cha afya cha Bugarama iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Josephat John, wengine ni Maofisa wa Serikali wilayani humo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Josephat John. (kushoto) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Mashine (Biohazard safety cabinet) mbili zenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa hospitali ya Manispaa ya kahama na kituo cha afya cha Bugarama mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga. Wengine ni Maofisa wa Serikali wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (aliyesimama) akiongea na wageni waalikwa katika hafla ya kupokea msaada wa mashine mbili za Biohazard safety cabinet zilizotolewa na Barrick kwa ajili ya hospitali mbili mkoani Shinyanga iliyofanyika mwishoni mwa wiki,wengine pichani ni maofisa waandamizi wa Barrick na Serikali mkoani humo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Josephat John (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Mashine (Biohazard safety cabinet) mbili zenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa hospitali ya Manispaa ya Kahama na kituo cha afya cha Bugarama mwishoni mwa wiki. (Wa tatu kutoka kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga. Wengine ni Maofisa wa Barrick na Serikali wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu, waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick, wakijiandaa kumpokea Mkuu wa Wilaya ya Kahama wakati wa hafla hiyo.
Mwonekano wa mashine ya Biohazard safety cabinet
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (Kulia) akisalimiana na Diwani wa kata ya Bugarama Prisca Msoma ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala katika hafla hiyo.
*
Mgodi ya Barrick Bulyanhulu, umetoa msaada wa mashine mbili za kuzuia kusambaa bacteria hatarishi kwenye maabara (Biohazard safety cabinet), kwa hospitali ya manispaa ya Kahama na kituo cha afya cha Bugarama kilichopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga, vyenye thamani ya shilingi ya milioni 30 ukiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya katika jamii.
Katika hafla ya kukabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki iliyofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Kahama, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu, Josephat John, alikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mheshimiwa Festo Kiswaga, vifaa hivyo vya kusaidia katika maabara.
Akiongea katika hafla hiyo Kaimu Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu Josephat John, alisema “Tunajivunia kutoa vifaa hivi maalum ili kuimarisha miundombinu ya matibabu katika jamii zinazozunguka migodi ya kampuni na huu ni mwendelezo wa jitihada za kampuni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma katika sekta ya afya nchini.”
Akipokea Mashine hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga ameishukuru Kampuni ya Barrick Kwaa kushirikiana na Serikali katika jitihada zake za kuboresha afya kwa jamii.
“Barrick hamjawa nyuma, mmekuwa mstari wa mbele kila wakati, serikali inapokuwa na jambo, mmekuwa mkifungua mikono yenu. Asanteni sana kwa kuiunga mkono serikali kwa jambo hili jema la kuleta vifaa hivi vya kisasa ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za maabara katika hospitali zetu”, alisema Kiswaga.
Kiswaga ametoa wito kwa wananchi kutunza afya zao pia ameutaka uongozi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama na Kituo cha Afya cha Bugarama kuhakikisha wanasimamia vyema matumizi na utunzaji wa vifaa hivyo.
Naye Diwani wa Kata ya Bugarama, Prisca Msoma, ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, aliipongeza kampuni ya Barrick kwa jitihada ambazo Imekuwa ikifanya kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye jamii ikiwemo kuboresha sekta ya afya.