Wachezaji wa timu za Wizara ya Elimu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakichuana katika mchezo wa kufuta kamba ambapo Wizara ya Elimu waliweza kuibuka na ushindi na kuweza kutinga hatua ya Robo Fainali katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga,mchezo huo ulikuwa ni hatua ya 16 bora
Wachezaji wa timu za Wizara ya Elimu wakichuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo Wizara ya Elimu waliweza kuibuka na ushindi seti 2-1,dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakichuana katika mchezo wa kuvuta kamba na kuweza kutinga hatua ya Robo Fainali katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga,
Wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa kwenye mchezo dhidi yao na Wizara ya Elimu ambapo walikubali kipigo cha seti 2-1.
Na Oscar Assenga,TANGA
TIMU ya Wizara ya Elimu ya mchezo wa Kamba Wanaume wametinga hatua ya robo fainali ya Mashindano ya Shimiwi ya mchezo huo baada ya kuikung’uta timu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwavuta kwa seti 2-1, katika mchezo wa uliokuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote mbili uliofanyika shule ya Sekondari Usagara.
Mashindano hayo yanaendelea katika viwanja mbalimbali Jijini Tanga yakihusisha michezo mbalimbali ambapo awali katika mchezo huo katika mzunguko wa kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka droo huku mzunguko wa pili wakiibuka na ushindi huo.
Katika mnchezo huo wa 16 bora ulikuwa wa aina yake kutokana na kila timu kutaka kupata ushindi na hivyo kuwalazimu kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanapenya.
Timu ya Kuvuta Kamba ya Wizara ya Elimu walionekana kuwa mwiba mchungu kwa wapinzani wao na hivyo kupelekea kupata ushindi huo wakiongozwa na wachezaji wao nmahiri Primius Mwalimu,Majaliwa Mkalama,Erick Charles,Fabian Haule na Fadhili Mwaijanda ambao walikuwa tishio kwa timu ya tume ya Taifa ya Uchaguzi.