Mhandisi Latifa Mzara kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa katika maadhimisho ya siku ya bahari duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya bahari duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza, kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu (sekta ya uchukuzi), Dakta, Leonard Chamuriho.
Muonekano wa meli ya Mv. Victoria ambayo ukarabati wake unaendelea na unatarajiwa kukamilika Machi mwakani na hivyo kuhuisha huduma za usafiri wa njia ya maji katika ziwa Victoria.
Inspekta Muchunguzi Kagenyi wa kikosi cha polisi wa maji mkoani Mwanza akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi) Mhe. Elius John Kwandikwa katika maadhimisho ya siku ya bahari duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Bwana Erick Hamisi akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua eneo kinapojengwa chelezo na ukarabati wa meli ya Mv. Victoria jijini Mwanza, kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu (sekta ya uchukuzi), Dakta, Leonard Chamuriho.