wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na mgeni rasmi katika maafali ya darasa la saba shuleni hapo
*****************************
shule zenye walimu wa kutosha pamoja na vitendakazi vya masomo mbalimbali hapa nchini zimeaswa kujijengea utaratibu wa kusaidia majirani zao ambao bado uwezo wao upo chini kwa kuwa lengo la ufundishaji wa masomo mbalimbali ni kuwakomboa watoto wa kitanzania ambao wanahitaji sana elimu kama mkombozi wao
endapo kama shule zitafanya hivyo ni wazi kuwa kiwango cha ufaulu kitaweza kuongezeka sana tofauti na sasa ambapo baadhi ya shule zinashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto mbalimbali
hayo yameeelezwa wilayani meru mkoani hapa na bw Revocatus Mwasambogo ambaye ni mkuu wa shule ya Steps Academy wakati akizungumza kwenye kusanyiko la maafali ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo
Mwasambogo alisema kuwa kila shule inapenda kuona kuwa taaluma au matokeo ya mwisho ya mithiani ni mazuri na shule zimeshika namba lakini bado shule hizo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo wakati mwingine ndio chanzo halisi cha kuwakwamisha katika harakati za kielimu
Alisema kuwa kwa sasa ni ngumu sana kwa changamoto hizo kuweza kuatuliwa zote lakini kama kukiwa na ujirani mwema baina ya shule na shule wataweza kuyafikia malengo ya kuwafikisha watoto katika viwango vya juu sana vya kitaaluma
“unakuta kuna shule ambayo ina uwezo mkubwa lakini nyingine haina mimi kama mdau wa taaluma nashauri kuwa kuwepo na wamasiliano mazuri ambayo yataweza kuasaidia hata kwa njia ya mithiani tu itatosha kuwajengea wanafunnzi uwezo wa kufanya vizuri zaidi”aliongeza
Katika hatua nyingine alisema kuwa tayari shule hiyo imeshaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia majirani zao lakini hata kufanya mithiani ya ujirani mwema ambayo italenga kuwasaidia wanafunzi hasa wale ambao wapo katika madarasa yenye mithiani ya mwisho
“tumejipanga kuhakikisha kuwa tunakuwa mfano bora wa elimu hapa Meru kwa kuweza kubadilishana mithiniani lakini pia hata walimu wetu kujitolea katika shule ambazo zina uitaji huo kwa kuwa wote tunajengas chungu kimoja cha elimu”aliongeza bw Mwasambogo
Awali akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao wameitimu elimu ya darasa la saba shuleni hapo Careen Mungure alisema kuwa pamoja na malezi na maadili mazuri waliyoapata shuleni hapo bado wazazi na walezi wana nafasi kubwa ya kuendelea kuwajenga zaidi ili waweze kufikia katika ngazi ya juu kabisa ya elimu