Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Sahy Solutions iliyopo Dubai,Husayn Mawji akizungumzia mkutano huo jijini Arusha
……………………………….
Julieth Laizer ,Arusha .
Ikiwa ni siku ya Pili ya Mkutano wa Shirika la Umoja wa Matiafa la utalii Duniani UNWTO kanda ya Afrika unaofanyika jijini Arusha, Tanzania imetumia mkutano huo kutangaza vivutio mbalimbali ilivyonavyo ikiwa ni mkakati wa kufikia watalii milioni Tano ifikapo 2025
Mkutano huo ambao unafanyika kwa siku tatu ukishirikisha wageni mashuhuri zaidi ya mia moja ikiwemo mazwaziri wa sekta ya utalii kutoka mataifa mbalimbali ulifunguliwa jana na Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi amesema kuwa, Tanzania inatumia mkutano huo kama njia ya kupata mikakati ya kufikia melengo iliyojiwekea kwenye sekta hiyo.
Maeneo yanayolengwa kuongeza watalii ni Utamaduni na misitu vitu ambayo vinapatikana nchini Tanzania ambapo Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania anasema tayari wameweka mikakati ya kuvutia watalii kwenye eneo hilo.
Nao baadhi ya wadau wa utalii wakizungumzia mkutano huo,Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Sahy Solutions kutoka Dubai,Husayn Mawji amesema kuwa mkutano huo umetoka fursa kubwa kuweza kwa nchi ya Tanzania kuweza kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Amesema kuwa,kupitia mkutano huo wataweza kwenda kutangaza vivutio vya utalii kwenye nchi mbalimbali ili kuweza kuongezeka kwa watalii zaidi na nchi kuweza kunufaika kimapato.
“Kwa kweli kikubwa kinachotakiwa hapa ni watanzania kujivunia kuwepo kwa vivutio hivi na kuhakikisha kila wanakuwa wanakuwa mabalozi wazuri wa kutangaza nchi yao kwani imejaliwa kwa vivutio vingi ambavyo unatakiwa kutangazwa zaidi ndani na nje ya nchi.”amesema Mawji.