****************
Na Lucas Raphael,Tabora
Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Tabora limedhamiria kutoa huduma bora na haraka kwa kuwaunganishia umeme wateja wake kwa siku 7 mara baada ya mteja kulipia .
Kauli hiyo ilitolewa leo octoba 6 mwaka huu na meneja wa shirika hilo mkoani hapa Mhandisi Khadija Mbarouk eneo la Kipalapala mjini hapa ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kimkoa.
Meneja huyo alisema kwamba shirika litaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ili kwenda na kasi ya maenendela kwa wananchi wanaoitaji huduma hiyo muhimu.
Alisema kwamba licha ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kimkoa shirika linakusudia kuendelea kutoa huduma rafiki kwa wateja wao.
“Tumeanza kutembelea wateja wetu ambao waliomba kuunginishiwa kwa muda mfupi na leo wameunganishiwa umeme hivyo kila mwananchi wa mkoa wa Tabora anastahili kupata huduma kwa haraka”Alisema.
Meneja huyo aliwataka wateja wao kuhakikisha wanapata huduma ya Nikonekt ambayo inamrahisishia mteja kujiunga kwa haraka na baada ya siku tatu hadi wiki inakuwa umepata umeme.
Naye mhandisi mwandamizi wa shirika hilo Hamisi Sosthenes alisema kwamba Tanesco itaendelea kutoa huduma kwa wakati na kasi na wateja wanapata furaha ya kuwa na huduma bora ya umeme .
Alisema kwamba wale wote watakao lipia huduma ya kuunginishiwa umeme wiki hii watapatiwa umeme ndani ya siku moja au mbili ili kufurahia umeme kwa maendelea ya Taifa.
Naye Msagigwa Mgulwa mteja aliyeunganishiwa umeme octoba 6 katika mtaa wa Songambele kata ya kipalapala alilishukuru shirika hilo kwa kumumpatia umeme kwa muda fupi baada ya kulipia huduma hiyo .
Alisema kwamba alilipia huduma hiyo ocotba 3mwaka huu na leo hii amewashiwa umeme .
Afisa uhusiano wa shirika hilo mkoani Tabora Witness Msumba aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika wiki la huduma kwa wateja ili kuweza kupata elimu na kuunginishiwa umeme kwa mfumo ya wa NIKONEKT ambayo ni njia rahisi ya kupata umeme .