Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Siha, Mhe. Dkt. Mollel amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati ya kuwekeza kwenye Tiba Asili baada ya kutoa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya utafiti kwenye eneo la tiba Asili.
Dkt. Mollel amesema hayo alipokuwa akizindua kituo cha Tiba Asili cha Tiba Jumuishi cha Afrika Alama kilichopo Kijiji cha Ngarenanyuki, Arumeru kituo ambacho kinatumia mitishamba kutoa huduma za Tiba ya Afya.
“Nimekuja ili kuionyesha Tanzania Hospitali ya Tiba Asili, Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 2.7 kwa ajili ya utafiti kwenye eneo la Tiba Asili, Rais Samia ana nia ya dhati ya kuendeleza Tiba Asili. Tuwatumie hawa watu(Kituo cha Tiba Jumuishi cha Afrika Alama) kuwajengea uwezo watu wetu ili tuwe na Tiba Asili kama hii katika Hospitali zetu ” alisema Dkt. Mollel
Pamoja na hayo, Dkt. Mollel aliongeza kuwa kuna majengo ya kutosha ya kutolea huduma katika hospitali zetu ambayo yamejengwa na Rais Samia Sukuhu Hassan.