Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Abdallah Mahmoud akizungumza mara baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa YMC wilayani Pangani kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi huo Mohamed Ratco kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Pangani
MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo akizungumza
Mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya Pangani Abdallah Mahmoud kushoto akipongezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wlaya ya Rajabu Abdurhaman wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na Waziri wa Maji
Mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya Pangani Abdallah Mahmoud kushoto akipongezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wlaya ya Rajabu Abdurhaman wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na Waziri wa Maji.
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akiwa na Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake Rajabu Abdurhamani wakiteta jambo wakati wa uchaguzi huo
Sehemu wa wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia uchaguzi huo
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia uchaguzi huo
**********************
Na Oscar Assenga,PANGANI
Abdallah Mahmoud amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani kwa kupata kura 411 huku akiwagaragaza wapinzani wake wawili waliokuwa wakiwania kiti hicho.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi Octoba Mosi mwaka huu kwa mujibu wa taratibu ndani ya chama hicho baada ya waliopo kumaliza muda wao wa kipindi cha miaka mitano ambao uliofanyika kwenye ukumbi wa YMC wila hapa Msimamizi wa uchaguzi huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mohamed Ratco alisema katika uchaguzi huo kulikuwa na wagombea watatu ambapo alisema kati ya kura 447 zilizopigwa mbili ziliharibika.
Aliwataja wagombea wengine na kura walizilopata kuwa ni Omari Ally aliyepata kura( 5) na Shafii Akida ambaye aliambulia kura (29 ) katika kinyang’anyiro hicho ambapo matokeo yake yalikuwa yakisubiriwa kwa shauku kubwa na wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi.
Wakati akitangaza matokeo hayo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu na wana CCM wilaya hiyo alimtaja Abdalah Mahamoud kuwa ndie mshindi wa kiti cha Mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya Pangani huku ukumbi mzima ukilipuka kwa shangwe .
Aidha pia Msimamizi huo wa uchaguzi aliwatangaza washindi katika nafasi ya tatu za wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa kutoka wilaya ya Pangani na kura zao kwenye mabano kuwa ni John Semkande (155),Mfaume Omari(210),Fatuma Suleman (229) ya kura halali 434 kati ya za awali 465 huku kura 31 zikiharibika na hivyo halisi kubakia 403.
Aliwataja wagombea ambao walibwagwa katika kinyang’aro hicho kuwa ni Seif Ally Said (135),Salim Ally (123),Amina Abdallah (120),Saumu Mbaruku (99),Seleman Rashid (84) na Omari Iddi (55).
Alisema pia katika uchaguzi huo walipatikana wajumbe wawili wa nafasi ya Mkutano Mkuu wa Mkoa ambapo kura zilizopigwa 445 zilizoharibika ni 47 hivyo kufanya kura halisi kuwa 398.
Aliwataja wajumbe hao wawili ambao walipenya katika michuano huo ambao ulikuwa na wagombea sita kuwa ni Rajabu Omari (160) na Fatuma Seif (223) huku wakiwabwaga wapinzania Omari Rahim(63),Mbwana Andrew(92).
Aidha kwa upande wa nafasi kundi la wakina Mama nafasi 4 ambazo zilikuwa zikiwaniwa na wagombea watano ambao walioshinda ni Mwana hasani Omari kura (204),Aisha Abdul (201),Amina Abdallah(195) na Amina Mohamed Salehe (192) huku Mwanahara Omari akigaragazwa kwenye kinyangany’iro hicho kwa kupata kura (95).
Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa zilikuwa 449 kati ya hizo 19 zikiharibika huku 430 zikiwa ni kura halali.
Hata hivyo Msimamizi huyo alisema kwamba katika nafasi ya kundi la wazazi watakaokwenda kuwakilisha wilaya hiyo kwenye Halmashauri Kuu Mkoa wa Tanga kuwa ni Twalibu Omari(216) na Salmini Abdi Omari(164) huku wakiwagaragaza wapinzani wao Omari Zuberi (83),Ally Sima (53),Rajabu Msomali (140),Shomari (142).